tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Saturday, March 2, 2013

wake za watu walikuwa kwenye semina

Kundi la wake za watu walikuwa kwenye semina
kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika
ndoa. Muwezeshaji akauliza, wangapi
wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha
mikono. Akauliza tena, 'Mara ya mwisho
umemwambia mumeo nakupenda lini?. Majibu
mbalimbali yalitolewa, Wengine wakisema Leo,
wengine Jana, wengine hawakumbuki. Kisha
akawaambia, kila mtu achukue simu yake halafu
amtumie mumewe text yenye maneno.
NAKUPENDA MPENZI, kisha wabadilishane simu.
Wakaambiwa kila moja asome majibu kwenye
simu aliyoshika, majibu yalikuwa kama
ifuatavyo;
Simu 1- Samahani nani mwenzangu?
Simu 2- He Mama Joji unaumwa?
Simu 3- Nami pia daima
Simu 4- Nini tena umeshagonga gari?
Simu 5- Sijakuelewa una maana gani
Simu 7- Umefanya nini tena? Leo
sitakusamehe
Simu 8-Chukua taim yako
Simu 9-?!?
Simu 10- Acha kuzunguka unataka shilingi
ngapi?
Simu 11 – Hivi naota?
Simu 12 – Kwa kweli leo usiponieleza hii mesej
ulikuwa unampelekea nani atakufa mtu shenzi
mkubwa
Simu 13 – Nilishakwambia usirudie kunywa
pombe au ntakuacha naona umechoka kuishi na
mimi
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania