tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Tuesday, November 11, 2014

Golden Words By A Wise Man

1. "If you want to change the world, do it when you are a bachelor. After marriage, you can't even change a TV channel"

2. "Listening to wife is like reading the terms and conditions of website. You understand Nothing, still you agreed..."

3. "Chess is the only game in the world, which reflects the status of the husband. The poor King can take only one step at a time...While the mighty Queen can do whatever she likes."

4. "All men are brave. Horror movies don't scare them...But 5 missed calls from wife...surely..."

Saturday, October 25, 2014

Wahehe

TANGAZO KWA WAHEHE WOTE:
Chuo kipya kabisa cha Kihehe kimefunguliwa Kihesa, Iringa.
(HEHE SKILLS AND TECHINICAL COLLEGE OF LIFE)

Kinatangaza kozi za mwaka 2015/2016 kama ifuatavyo,
1. Kugema ulanzi miezi 6
2. Kusokota kamba za kujinyonga miezi 9;
3. Kuchagua mbwa anaefaa kuliwa na mapishi yake miezi 8;
4. Kuongeza hasira miezi 10-12Atakae.
 jiunga mapema atapewa kozi ya upishi wa Mkunungu pamoja na uoshaji wa Mbeta.

Wasambaa

Wasambaa wanapenda sana kazi zao hasa udeeva (udereva). Ukimkuta msambaa msukuma mkokoteni muulize kazi yake utasikia mimi deeva.

Wazaramo

siri ya wazaramo kutopenda shule ni kutokana na wao kuzaliwa Da es salaamm hivyo hawaoni sababu ni kwa nini waende shule, bali wa kwenda shule ni watu wa mikoani sababu wao wanasoma ili waje Dar es Salaam.

utasikia wanasema

wazaramo: wewe unasoma uje darichalama, mie nisome niende wapi?


(wakati ule karibu kila kitu kilikuwa Dar, ajira Dar, Chuo Kikuu Dar, nk.)

Mfupi

Rafiki yake Jost ni mfupi mpaka akikaa kwenye kiti badala ya kukunja nne, yeye anakunja mbili

Wednesday, September 24, 2014

M-pesa na tigo pesa

Jost: Dada Mambo?
Chaupele: Powa.
Jost: Samahani, nimevutia na wewe nataka tuwe marafiki, Hivi Uko Facebook?
Chaupele: Hapana.
Jost: Twitter?
Chaupele: Sipo.
Jost: Whatsap?
Chaupele: Sipo.
Jost: Instagram?
Chaupele: Sipo.
Jost: Eeeeh Sasa upo kwenye mtandao gani sasa?
Chaupele: Niko M-pesa na tigo pesa.

Wednesday, September 17, 2014

huna uwezo wa kupata mimba

Binti mmoja aliamua kwenda kwa dakitari baada ya kuona hapati mimba, alipofika na baada ya vipimo.
Dakitari: binti inaonyesha wewe ni mgumba kwa hiyo huna uwezo wa kupata mimba.
Binti: jamaniii (huku akianza kutokwa na machozi).
Dakitari: usilie ngoja tujaribu kuangalia chanzo cha tatizo ni nini tuone kama kuna msaada.
Binti: naomba unisaidie.
Dakitari: usijali, lakini hili tatizo linaweza kuwa la kurithi, kwani mama yako aliwahi kuzaa?
Binti: sijui labda nikamuulize.
Dakitari: …………….

Binti:……………

Chaupele

Jost: mambo mrembo, mbona kimya?
Chaupele: unanitaka unagari lakini?
Jost: gari?
Chaupele: ndio gari.
Jost: sina gari.
Chaupele: basi acha kunifuata fuata hunifai
Jost: vipi kwani we unalo?
Chaupele: sina gari.
Jost: una sehemu ya kuosha magari au garage?
Chaupele: sina
Jost: baba yako analo gari?
Chaupele: Hana gari.
Jost: sasa wewe mazoea ya kupanda gari umeyatoa wapi?

Chaupele: nyooooo….. mbwa weee unikome!

baba ni mbahili sana

Baba alikuwa na tabia ya kulala na dada wa kazi, siku moja mtoto wake wa kiume akamfumania:
Baba: Mwanangu, ebu chukua hii Shs 500 halafu usimuambie mama yako kuwa nimelala na dada.

Mtoto: sitaki, we baba ni mbahili sana, mbona mama akilala na mlinzi ananipaga Shs. 1,000?

Monday, July 14, 2014

mara ya mwisho kuongea na boyfriend wako lini?

binti mmoja wa kidato cha kwanza akiwa anatoka shule simu yake iliita alipoitoa akaona ni namba ngeni kwake. alipopokea akakutana na sauti ya kiume na ikamuuliza
mwanaume: Mara ya mwisho kuonana na boyfriend wako ilikuwa lini?
bint: jana jioni nikiwa natoka shule.
mwanaume: kumbe we mtoto una wanaume ngoja urudi nyumbani utanitambua, maana mama yako alikuwa ananiambia nambishia.
bint: baba nilikuwa natania tu, nilijua ni wavulana wanaonisumbua ndio maana nikasema hivyo.
baba yake akakata simu, yule binti akiwa anakaribia kufika nyumbani simu ikaita tena na ninamba mpya na tofauti na ya mwanzo, alipopokea akasikia tena sauti ya kiume.
mwanaume: una boyfriend?
binti: hapana sina
mwanaume: kumbe hunipendi eeh yaani unanikana?
binti: samahani mpenzi nilijua baba yangu, nakupenda sana na ndio maana nikatoroka jana jioni na kuja kwako.
mwanaume: pumbavu, utanikoma nilitaka kupata ushahidi zaidi, juu ya huo upumbavu wako.
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

kanyonyeshe mtoto

MKE: Mbona hawa Brazil hawamchezeshi Neymar ?
MME: Aliumia mechi iliyopita, hawezi kucheza
MKE: Mbona hawajamkodiMESSI??
MME: Hairuhusiwi kukodi... izo sio nyumba za kupanga
kwamba unahamia tu,mpaka uwe una uraia waNchi
yako.
MKE: Mbona hadi wanawake wanacheza umo
uwanjani?
MME :Wapo wapi hao wanawake?
MKE: Si hao wa Brazil wenye
nywele ndefu?
MME: hapana hao ni Wanaume wanaitwa David Luiz na
WILLIUM
MKE: Mbona hao wengine wanapiga Penati 5
wenyewe? eti Refa anapendelea?
MME: Hakuna Penati hapo ni magoli,Brazil wamezidiwa
wanafungwa.
MKE: Mbona Goli 7 ni nyingi na ni Dk ya 80, kwanini
refa
hamalizii tu hapo si bingwa alishajulikana.
MME: Sheria ya mpira mpaka Dk 90 zitimie..
MKE: Huu si mpira wa miguu??
MME: Ndio we unaonaje?
MKE: mbona huyo mwingine anadaka na mikono?
MME: huyo ni kipa
MKE: kwanini huyu Kipa wa Brazil asikimbie na mpira
hadi goli
jingine alafu afunge apunguze magoli au hajui huo
ujanja?
MME: kanyonyeshe mtoto ameamka...
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

Wednesday, July 9, 2014

Unaumwa nini

Kuna babu mmoja alikutwa stendi ya mabasi analia sana. Wasamaria wema wakaamua kumsaidia yule babu lakini kila walipokuwa wakimwuliza, “Babu unalilia nini?” akawa hasemi anaendelea kulia tu, wasamaria wema wakaamua kumbeba hadi hospitali. Walipofika hospitali daktari akamwuliza babu tatizo lake ili aweze kumsaidia,
Daktari: Mzee unaumwa nini?
Babu: (Akaendelea kulia kwa muda)
Daktari: Eti babu yangu nini kinakusumbua? Unaumwa nini nikutibu?

Babu: SIUMWI ILA VIATU VINANIBANA!!!

wamekubaliana na baba

Baba, mtoto wake na jiran yao,walikuwa wawindaji wa wanyawa pori, kwa kutumia mtego mkubwa wa nyavu (IKILA). Kawaida ya mtego huo mmoja akae mwishoni mwa urefu na mwingine nae mwshoni vilevlie. Sasa mzee akawa atatafuta wanyama kila kichaka, bahati nzuir akatokea mnyama aina ya NGIRI, mnyama huyu huwa ana meno mawili yaliyo tokokeza nje, akaelekezwa na mzee kwnye mtego, akalenga upande wa mtoto, badala ya kumuuwa, akamkwepa. Alpoulizwa vipi wewe? kasema, mnyama mwenyewe alikuwa anacheka, mi nikadhani yawezekana kuna maelewano wamekubaliana na baba.

Dawa ya kuacha Pombe

Mlevi nae akaenda kupata dawa ya kuacha pombe, akambiwa awe anameza vidonge viwili mara tatu kwa siku, akamuuliza dr, hizi dawa kwani zinamadhara nikimeza alafu nikanywa pombe?

dawa ya kuacha bangi

Mshikaji alienda kwa Dr kupata dawa ya kuacha bangi, dr akamwambia awe anameza mara tatu kwa siku, mshikaji akamuuliza niwe nameza baada ya kuvuta bangi au kabla?

kama Mvua inanyesha

Jamaa alikuwa Ktandani na mke wa mtu mwenyewe akarudi na kugonga Mlango Mke akamwambia Jamaa pitia dirishan Kimbia, jamaa akaanza kubisha eti nje Kuna Mvua, Mwanamke akamwambia Mme wangu ana hasira na ana Pisto, jamaa akachukua Nguo zake na kuruka dirishani na Kukimbia kufika Barabarani akakuta watu wengi wanakimbia wako kwenye Mashindano ya mbio nae akajiunga mmoja akamuulza mbona unakimbia Uchi? Jamaa akajibu napenda sana kukimbia hivi najisikia poa, mwingine akamwambia ndo ukimbie Nguo umebana kwapani? Akajbu sasa niziweke wapi? Mwingine akamuulza kwa hiyo kila ukiwa unakimbia unavaa Kondom? Jamaa huwa navaa kama Mvua inanyesha.

kufanyiwa usaili

Jost alikuwa anatafuta kazi sana... akaenda ofisi moja na kuanza kufanyiwa usaili,
Afisa: una akili timam
Jost: ndio, ninazo.
Afisa: 1 + 1 =?
Jost: 2
Afisa: nani alimuua Abraham Lincorin?
Jost: mhh! Sijui
Afisa: okey! Kalifanyie kazi hilo afu kesho urudi hapa...
Jost akaenda kwa rafik yake, akaulizwa umepata kazi?

Jost akajibu “ndio, tena nzito kweli, nashughulikia kesi ya mauaji.”

Saturday, June 14, 2014

hai beibi

Sista duu amesmama kituoni kwa
pozi zote mara daladala
ikatokea!..akaismamisha kwa mnato
na kupanda!...
Konda: "hai beibi"
Sista duu: (kimya) huku akitingisha
kichwa
Konda: "hai beibi"
Sista duu: "hebu ntolee kelele,kwani
salamu lazima"
Konda: "sijakusalimia nimekwambia
daladala haibebi"

DENI WATALIPA WAJUKUU ZAKO

Kuna hotel imeandikwa "KULA UWEZO WAKO DENI WATALIPA WAJUKUU ZAKO". Jamaa akaingia akajivinjari mlo kinoma ilipoletwa bili akaruka! Jamaa:Oya mhudumu pale nje mmeandika vipi au hujui kuxoma au huelew maandish? Mhudumu:Najua na nimeelewa, ila hii sio bili yako alikula babu yako..! Jamaa akazimiaKuna hotel imeandikwa "KULA UWEZO WAKO DENI WATALIPA WAJUKUU ZAKO". Jamaa akaingia akajivinjari mlo kinoma ilipoletwa bili akaruka! Jamaa:Oya mhudumu pale nje mmeandika vipi au hujui kuxoma au huelew maandish? Mhudumu:Najua na nimeelewa, ila hii sio bili yako alikula babu yako..! Jamaa akazimia

WATCHING A FOOTBALL

WATCHING A FOOTBALL GAME WITH A
GIRL IS STRESS.
girl- hey beib, who is that guy? is he
chris brown?
BOY- no, thats theo walcott!
girl- oh beib, whats that yellow card for?
BOY- thats sounds a warning to a
player and a red card is to sent a
player off the field.
girl- what about green card?
BOY- nothing like that!
girl- hey beib, i want arsenal to win
the world cup, my friend daily
supports brazil but i dont like that.
boy- silent
girl- WHO IS THAT COACH?
boy- arsene wenger.
girl- ahaa. . so it seems the other
coach is manchest wenger? ?. . .
boy

Wamenikata kidole

Watoto wapo hospitali,
mtoto wa kwanza kamwona mwenzie analia
ikawa hivi :-
Mtoto wa 1: Unalia nini?
Mtoto wa 2: Nimekuja kupima damu.
Mtoto wa 1: Ndio sababu unalia?
Mtoto wa 2: Wamenikata kidole changu.
Mtoto wa 1 Na yeye kaangua kilio, kilio balaa zaidi ya mwenzie!!.
Mtoto wa 2: Unalia nini?
Mtoto wa 1: Nimekuja kupima mkojo...!!

Friday, June 6, 2014

SURA YA MZIKAJI

Katika kijiji cha Matare wilaya ya
Mugumu Serengeti, bwana
Wambura alikamatwa kwa kesi ya
kusingiziwa na kuhukumiwa kwenda
jela miaka mitatu.
Huku nyuma akiacha mke na
watoto wanne waliokuwa
wanasoma. Hukumu hiyo ilimtesa
sana kichwa chake, alitamani kila
mtu anayemhisi kuwa ana makosa
aingie katika moyo wake na
kuupata ukweli.
Alilia na umaskini wake, lambda
angepata wakili mzuri angeweza
kumtetea, kumkosa wakili
kukahalalisha kifungo hicho!!
Alikwenda gerezani huku akiumia
sana rohoni. Aliyaanza maisha
mapya kwa shida sana, akawa
mnyonge kila mara na mwili
ukapoteza afya kiujumla.
Huko gerezani alifanikiwa kupata
rafiki aliyekuwa na cheo ama
jukumu la uzikaji wa wafungwa
hasahasa ambao hawakuwa na
ndugu ama ambao ndugu zao huwa
hawajitokezi pale gerezani.
Mzikaji alijaribu sana kumtia nguvu
Wambura na kumwaminisha kuwa
hiyo ilikuwa hatua tu ya maisha
anapaswa kuizoea na siku moja
ukweli utajulikana tu! Bwana
Wambura maneno ya mzikaji
hayakumuingia kabisa.. alizidi
kunyong'onyea.
"Siwezi kuvumilia kukaa gerezani
miaka mitatu…..kama unajali kilio
changu nisaidie nitoroke kwa
namna yoyote ile ndugu yangu!!"
Wambura alimsihi mzikaji.
SIKU MOJA mzikaji akamwambia
Wambura kuwa msaada
umepatikana. Lakini yataka moyo!!
"Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu
nitoke humu!!" alijibu kwa msisitizo
huku akimtegea sikio mzikaji.
"Msaada pekee wa kukutorosha
humu ndani ni kwa njia ya jeneza…
yaani mfungwa akifa mimi
nakuunganisha naye kwenye
jenerza….." akashusha pumzi kisha
akaendelea "Wewe ukisikia kengere
ya msiba, njoo mara moja kwenye
chumba cha maiti, utakuta tayari
sanduku liko katikati ya chumba
linakuwa halijafungwa, funua
kifunioko ingia ndani yake ulale
pembeni ya maiti kwani sanduku
huwa kubwa la kutosha kila aina ya
maiti na hata miili miwili inaingia.
Kisha nitakuja na kulipigilia
misumari. Baada ya mudap
tutalipakia kwenye gari na kutoka
kwenda nje ya gereza makaburini
nikiongozana na baadhi ya
wafungwa na maaskari magereza.
Tutakuzika huko lakini baada ya
dakika 20 hadi 30 nitarudi
kukufukua. Hautaweza kushindwa
kupumua kwa dakika hizo, utatoka
ukiwa huru."
JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini
lilimtisha sana Wambura. Hata
hivyo akaona afadhali afanye hivyo
kuliko kukaa gerezani miaka mitatu
bila kosa.
Siku moja akasikia kengele ya
msiba. Akafanya kama
alivyoelekezwa na mzikaji. Akaenda
na kuingia chumba cha maiti. Kweli
akalikuta sanduku, akiwa na hofu
kuu akaingia na kulala pembeni ya
maiti iliyokuwepo. Mara akasikia
mtu ameingia na kulipigilia
msumari sanduku. Muda mfupi
baadaye sanduku likainuliwa na
kuwekwa kwenye gari.
Gari ikatoka nje ya gereza hadi
makaburini. Sanduku likashushwa
na kuwekwa kaburini na kuanza
kufukiwa.
Wambura alijitahidi sana kuvumilia
japo hofu ilizidi kutanda.
Alimtegemea sana mzikaji na
alianza kumuona mkombozi wa
maisha yake.
Kama alivyoambiwa, akasubiri
dakika kumi, ishirini.. zikapita
kimya!!
Dakika thelathini kimya. Joto nalo
likazidi kuongezeka.
"Nitavumilia hadi afike…"
alijisemea kisha akajiongezea kauli
ya ujasiri.
"Kama nilitakiwa kuishi gerezani
miaka mitatu kivipi dakika kadhaa
za hapa kaburini"
KWA kuwa alishakaa gerezani kwa
muda kiasi akatamani kujua
aliyekufa ni nani… ni kwewli
aliogopa kuitazama maiti lakini
aliona kama inatisha zaidi ikiwa
imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi.
Akaifunua upande wa usoni… Kwa
kuwa kulikuwa na giza nene
alikodoa sana macho kuitazama.
LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA
NA SURA YA MZIKAJI!!!

Saturday, May 31, 2014

ndoto zao za baadae

Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.

MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?

JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.

MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?

ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.

MWAL: Na wewe James??

JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe......"Akameza mate kisha akaendelea....

"Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali."

MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??

JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!

Friday, May 23, 2014

nani msaliti

Hebu nisaidie kuamua kesi hii. Mtu na mkewe wamelala, katikati ya usiku mke akaweweseka "wewe amka tena uondoke mume wangu anakuja" Ghafla mume nae akakurupuka akanyakua nguo zake na kurukia dirishani. Kufika nje mume akakumbuka aaah!! Kumbe leo nimelala nyumbani. Je! Kati yao nani msaliti wa mwenziwe?

kiingereza

Vipi tatizo lako la kiingereza limeisha au bado? Unakumbuka ile siku uliyoenda hoteli ya kitalii ukashindwa kuagiza kuku. Ila ulipoona yai ndipo ukajitutumua na kusema;
"I need mother of this"

phonebook

Phonebook ya mmama wa kichaga:
1.dokta wa ng'ombe
2.masawe muuza pumba
3.pickup ya majani
4.kijana mkata majani
5.juma muuza vifaranga
6.fundi banda
7.machine ya kusaga
8.muuza maparachichi
9.muuza bucha
10.fundi garage
11.kijana muuza duka
12.mama muuza soko
13.dereva tax
14.n.k
phonebook ya mama wa kizaramu utakuta
1 .msasambuaji
2.mpiga ngoma
3. muuza shanga
4. mganga wa jadi
5. muuza urembo

Thursday, May 22, 2014

Michepuko noma

Mume: My wife Let's close our eyes and pray....
"Lord I pray for Grace, I pray for Mercy, I pray for Patience, I pray for Joy, I pray for Love, I pray for Faith, I pray for Happiness, I pray for Hope, I pray for Glory, I pray for......"

Mke: Heeee sasa ndo unamaanisha nini, unanichezea sio? Asiyekuwa na wapenzi ni nani?

"Na mimi I pray for Prosper, I pray for Kelvin, I pray for Omari, I pray for Mbelwa, I pray for Noah, I pray for David, I pray for Daniel, I pray for Umande, I pray for wengine wote niliowasahau majina yao.."

bodaboda inaweza kuwa ambulance

Usije kariri hata siku moja kwamba 3x1 ni sawa na 1x3 kama huamini kuwa si sawa fanya hivi kama una malaria kali nenda hospital wakikupatia qunine wakakwambia meza 1x3 wewe meza 3x1 hapo ndo utajua kwamba bodaboda inaweza kuwa ambulance.

New Job Titles

Stop calling others with old titles, just use the new ones.

Garden Boy- Landscape Executive and Animal Nutritionist

Receptionist - Front Office Manager/ Office access Controller

Typist - Printed Docoment Handler

Messenger - Business Communications Conveyer

Window Cleaner - Transparent Wall Technician

Temporary Teacher - Associate Tutor

Tea Boy - Refreshments Manager

Garbage Collector - Environmental Sanitation Technician

Guard - Theft Prevention ana Surveillance Officer

Prostitute - Practicala Sexual Relations Officer

Thief - Wealth Distribution Officer

Driver - Automobile Propulsion Specialist

Maid - Domestic Manager

Cook - Food Preparation Officer


Gossiper - Research Manager

kama mke wangu

Jamaa alikuwa amekaa ndani ya club. Changudoa akamsogelea na kumwuliza,
"Unataka mambo yetu?"
Jamaa akamwambia, "Ndio. Lakini, unaweza kunipa kama mke wangu?"
Changudoa akamjibu, "Hapa usipime. Mimi noma .... Ntakupa mpaka mkeo usimkumbuke! Kwani huyo mkeo anakupaje?"

Jamaa akamjibu, "Mke wangu ananipa bure." Changudoa, "Nyoo! Fisadi wa biashara za wenzio ...

uamuziii gani utachukua

ukiwa huna hili wala lile unashtuka na kofi moja zito la uso linakupeleka kufumba macho, kabla huja kaa sawa inakuja ngumi ya uso halafu unasikia sauti ya anae kupiga ikisema NILIKWAMBIA IPO SIKU NITAKUKAMATA TU ile kuinua sura unakutana na sura usiyoifahamu kabisaaaaa!!! halafu na yeye anashtuka baada ya kukuona kisha anakwambia SAMAHANI NIMEKUFANANISHA


Je ni uamuziii gani utachukua....

fundi KASAMBALA

Mfanyakazi wa mochwari aliona maiti ina sehemu za kiume mkubwa kuliko kawaida, akaamua kuzikata ili akamuoneshe mkewe,mkewe kuuona ule uume akatahamaki, mtumee inamaana fundi KASAMBALA amekufa!!!? Jamaa akazimia palepale na inasemekana kila akimuona mkewe anazimia tena......!

ugonjwa huu mbaya

bibi alikua anafua nguo za mjukuu wake ambae anaugua ukimwi katika fua fua akakutana na bikini, bibi akasema ugonjwa huu mbaya unakondesha mpaka chupi.

dola 20

Mlev huyu kila anapoenda kilabun lazima anywe zimshinde had kutapika...mke wake hapend sana kufua mashati alotapikia...akawa anaondoka tena ..mke wake akamsisitzia asitapikie shati...jamaa akalewa akajisahau akatapika...akaanza kujilaumu...rafiki ake akamtell...chukua hio dola 20 mpe mkeo afu umtel ka kuna mlevi kakutapikia na akakupa dola 20 ya kusafishia...jamaa akarudi hom kumkuta waifu anamsubiri...
Mke: ehe! Jitu zima ovyo...umejitapikia tena kwa shat mpya we vip!!
Jamaa: hapana mke wangu,,,kuna mtu kanitapikia afu kasema uchukue hii hela ya kufulia...
(mke akachukua hela kukuta ni dola 20 mbili tofauti)
Mke: sasa mbona zipo mbili?

Jamaa: oh! Na hio ni yule mlevi mwingine alieninyea ndan ya suruali...

Rubani wa kigeni

Rubani mmoja wa kigeni alikuja katika mbuga za Tanzania kwa ajili ya uwindaji nyama pori.

Akawaajiri wawindaji wawili akawapeleka kwa ndege hadi mbugani akawaacha wawinde ili akirudi na awachukue pamoja na nyama warudi mjini.

Aliporudi baada ya wiki moja akakuta wamewinda nyama nyingi kuliko uwezo wa ndege yake ndogo, rubani akaiangalia ile nyama kisha akawaambia “hatuwezi kuibeba nyama yote hii pamoja na nyinyi ndege itazidiwa uzito, itabidi nusu ya hiyo nyama tuiache”. Wawindaji wakasema “Mbona hata mwaka jana pia tulibebe nyama nyingi kama hii, na sisi wa wili na rubani aliyetuajiri katika ndege yenye uwezo kama wako, tuibebe tu”.

Rubani akasitasita lakini akaona awaamini akasema ” sawa haina tatizo, kama mlibeba mwaka jana basi tubebe tu na mwaka huu”

Wakapakia nyama na wawindaji wakapanda kisha ndege ikaondoka, ilipofikia katika mlima wakaribu ndege ikashindwa kuenda juu zaidi kutokana na ule mzigo na hatimaye ikapata ajali katika mlima, kwa bahati nzuri wote walipata majeraha tu hawakufa.

Rubani: (huku akiwa ajielewi kidogo) Hapa tulipoangukia ni wapi?


Mwindaji mmoja: usijali, nahisi hapa ni karibu na pale tulipoangukia mwaka jana

sijazimia nimejikojolea

Jamaa alikuwa ana tabia ya kukojoa kitandani baadhi ya siku.
Akafikia kuoa. Katika ya siku za mwanzo baada ya harusi, siku moja kama kawaida yake alijikojolea.
Akapiga kelele “Mungu wangu eee”.
Mke wake akashtuka, akamuuliza: Vipi mume wangu?
Mume: Hivi mke wangu ungeota unataka kuliwa na mamba, chuwi na simba kwa wakati mmoja ungefanyaje?
Mke: Ningezimia kabisa.

Mume: Basi mwenzio sijazimia nimejikojolea.

Hata sijui

Mlevi mmoja alianguka toka kwenye ghorofa, fasta fasta watu wakamfuata kumsaidia, wakamuuliza VP IMEKUAJE?
Mlevi akajibu:

”HATA SIJUI NA MIE NDO NAFIKA SASAHIVI…”

Padre na Mbunge

Padre mmoja mzee alistaafu na wanaparokia walimfanyia sherehe kubwa. Katikasherehe hiyo, mbunge wa eneo hilo alipangwa kutoa hotuba ya shukurani yakumuaga padri huyo kwa niaba ya wanaparokia wote. Bahati mbaya, mbungealichelewa kufika ....
Mc akamwomba padri aseme machache wakati wanamsubiri mheshimiwa mbunge.
Padri hakujipanga kusema kitu lakini kwa kujitahidi, aliongea.
"Wapendwa, naikumbuka sana siku nilipofika katika kanisa hili kwa mara yakwanza, ila nilipata mshangao siku nilipoanza kuungamisha. Mtu wa kwanzakabisa kumuungamisha alinishangaza sana. kwani alisema amemwibia bosi wakeTV, amemwibia ndugu yake pesa za urithi, amezini na jirani yake, na piakatembea na house girl wake. Nikapata picha kuwa kumbe watu wa kanisa hilindivyo walivyo, nikasikitika sana. Kumbe nilifikiria tofauti. Kwani baadayenikakuta kumbe watu wa hapa ni wazuri sana na hawatendi dhambi mara kwa marana ni wastaarabu sana".

Mara mheshimiwa mbunge akawasili, padri akakatisha maongezi na mbungeakaanza kuhutubia. "Ndugu wapendwa, naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kwaninilikuwa na majukumu makubwa ya kiserikali. Pia ninayo furaha kubwa kwakunipa nafasi hii kuhutubia kwa niaba yenu. Mimi nina bahati sana kwani padri huyu alipokuja hapa, mimi nilikuwa mtu wa kwanza kwenda na kuungama kwake....

Wednesday, May 21, 2014

ndiye aliyegundua

ni kweli kwamba
Mtenda dhambi ndiye aliyegundua "Kutubu?"

mfupi nae akagundua "ngazi"?

Mvivu ndiye aliyegundua "Kuiba"?

Mpweke ndiye aliyegundua "Kupenda"?

Mjinga ndiye aliyegundua "Kusoma"?

Masikini ndiye aliyegundua "Kuombaomba"?

Asiyejua kutongoza ndiye aliyegundua 'kubaka'?

Na malaya ndie alie gundua 'condom'?

sasa nikuulize mwenzangu, Je wewe mpaka leo hii umegundua nini?Usicheke tusaidiane

Tuesday, May 20, 2014

China phone

l got angry and sold my Blackberry phone because it was eating much of my airtime and data. I then went and bought a China phone but am now in a very big trouble.
1. It gets full after 3 minutes of charging.
2. The phone has TV, Touch screen, Nail cutter, firelighter etc.
3. Text messages can be written with a toothpick.
4. It has some spelling mistakes, it is written NokLa instead of Nokia.
5. When an aeroplane passes by it records "one missed call".
6. When a big truck hoots; it records "charger connected"
7. When a Chinese man passes by you it says "one Bluetooth device found"
8. When a cute girl passes by me, it says "Ur favorite food found"
9. When an ugly girl passes by me, it says, "Virus detected".
Please, I want to sell it,do u want it?

Smartphones

Smartphones has already replaced camera, calendars, notebooks, alarm clocks etc in our life,

Don't let them replace you in your family.

hali ya baba nayo siku hizi si nzuri sana

Familia moja ilishangazwa pale
walipopokea jeneza la marehemu mama yao


aliyefariki nchini Marekani. Lilitumwa na mmoja ya watoto wake wa kike.

Mwili ndani ya jeneza ulikuwa umesongwa sana
ndani ya jeneza kiasi

kwamba uso wa marehemu ulikuwa umegusa kioo cha jeneza!

Walipofungua jeneza, walikuta barua juu ya merehemu, iliyosomeka namna

hii:

'Wapendwa ndugu zangu, nimeutuma mwili wa mama yetu kwa ajili ya

mazishi, kwani imekuwa siku zote hamu yake kubwa kuzikwa nyumbani Machame,
katika nyumba ya ukoo. Samahani sikuweza kuja na mwili kwani

nimenyimwa likizo kwani kuna upungufu wa wafanyakazi hapa kazini mwezi

huu.

Ndani ya jeneza, chini ya mwili wa mama, kuna makopo 12 ya samaki wa

makopo, paketi 10 za supu ya Royco na chupa 8 za jam ya maembe. Mgawane

hivi kwa jinsi mtakavyoamua nyinyi.

Katika miguu ya mama kuna pea moja ya viatu vya Reebok namba 9 kwa ajili

ya mtoto mkubwa wa Mushi. Pia, kuna pea mbili za viatu kwa ajili ya

watoto wa Urassa na Kwayu, natumaini nitakuwa sijakosea namba za miguu.

Nimemvalisha pia mama American T-shirts 6, kubwa kabisa ni kwa ajili ya

Manka, na zinazobaki ni za watoto wake. Hizo jeans mpya 2 ambazo mama

amezivaa ni za wavulana. Hiyo Swiss watch mkono wake wa kushoto ni

zawadi ya Koku kwa ajili ya sikukuu yake ya kutimiza miaka 21. Anti

Rebeka, hizo heleni, mkufu na pete ambazo mama amevaa ni zako.

Hizo soksi 6 ambazo mama amevaa wagaiwe wajomba. Tafadhali mgawane kama

nilivyosema na kama kuna kitu kingine mnahitaji, basi mnieleze kwani

hali ya baba nayo siku hizi si nzuri sana.

Dada yenu mpenzi,

Mama Manka

Fomu toka kwa baba mkwe mtarajiwa.

FOMU YA MAOMBI YA KUMUOA BINTI YANGU

KIJANA, JAZA FOMU HII KWA MWANDIKO WAKO MWENYEWE NA KWA HERUFI KUBWA.

Mimi ......................., natuma ombi la kumuoa binti yako. Nina umri wa miaka ..............


TAFADHALI JIBU MASWALI YAFUATAYO KWA UAMINIFU.

1. Huwa unahudhuria ibada? Ndiyo/Hapana
2. Una Masters au PhD? Ndiyo/Hapana
3. Una undugu au urafiki na tajiri yeyote mkubwa mjini? Ndiyo/Hapana
4. Mshahara wako una tarakimu 7? Ndiyo/Hapana
5. Unamiliki nyumba? Ndiyo/Hapana
6. Una gari? Ndiyo/Hapana

KAMA KATIKA MASWALI 6 HAPO JUU KUNA LOLOTE UMEJIBU HAPANA BASI USIENDELEE KUJAZA FOMU HII NA FUTA NDOTO ZA KUMUOA BINTI YANGU. KAMA MAJIBU YAKO YOTE NI NDIYO ENDELEA KUJAZA FOMU.

1. Kwa kutumia maneno yasiyopungua 50 elezea hasara za kuchepuka katika ndoa.

--------------------------------------
----------------------------------------------------------------------------------

2. Kwa kutumia mchoro elezea namna gani unaweza kuwapa heshima baba na mama mkwe wako.

3. Mfano mkeo akikwambia "Mume wangu nahitaji hela ya kwenda saluni" utamjibu vipi?

-----------------------------------------

4. Elezea sababu 10 za ndoa nyingi kuvunjika.

5. Elezea maana ya maneno "mume mwema" kama unavyoyafahamu wewe binafsi.

6. Wazazi wako wamefunga ndoa? Ndiyo/Hapana. Kama ndiyo, ndoa yao ina muda gani?

Kama umri wa ndoa ya wazazi wako ni mdogo kuliko umri wako elezea kwa nini ulizaliwa nje ya ndoa.

7. Elezea maana ya "Mume wangu urudi nyumbani mapema" kwa maneno yasiyopungua 100.

8. Toa sababu 3 ambazo zinaweza kumfanya mwanaume asilale nyumbani kwake na mkewe.

9. Ndoa ikivunjika, unadhani nani mmiliki wa watoto kati ya baba na mama.

JIBU MASWALI HAYA KWA KUANDIKA NDIYO AU HAPANA.

1. Unakunywa pombe?
2. Unavuta sigara?
3. Una hasira za karibu karibu?

HII NI SEHEMU YA MWISHO LAKINI MUHIMU KAMA NYINGINE ZOTE HAPO JUU

1. Lini uko tayari kuja kwangu kufanyiwa intaviu?

----------------------------------------

2. Siku na muda gani unadhani ni sawa kumuhoji baba au mlezi wako wa kiume kuhusu hii nia yako?

-----------------------------------------
3. Siku na muda gani unadhani ni sawa kumuhoji mama au mlezi wako wa kike kuhusu hii nia yako?

-----------------------------------------

4. Siku na muda gani unadhani ni sawa kumuhoji kiongozi wako wa kidini kuhusu hii nia yako?

-----------------------------------------

5. Tafadhali bandika picha yako ya rangi ya siku za karibuni ambayo itarushwa katika magazeti na mitandao ya kijamii ili kujua kama una wapenzi wengine.

Weka sahihi hapa:

-------------------------

Rudia kuweka sahihi hapa:

----------------------------------

Asante kwa kuonyesha nia ya kumuoa binti yangu. Muda wa kupitia maombi yako ni miezi 6. Utajulishwa kama tu utafanikiwa.

Niandikie anuani zako hapa chini ili niweze kukufikia kama nitakuwa na maswali zaidi.

E-mail: _________________
Simu: __________________
Facebook: ______________
WhatsApp: ______________
Twitter: _________________
Instagram: _______________
LinkedIn: _________________
BBM PIN: ________________

Nakupenda mke wangu

Mdada mmoja alitaka kujua kiasi gani
anapendwa na mume wake, hivyo akataka kujua
mumewe atafanya nini endapo ataamua
kuondoka na kumuacha!
Mwanamke huyo akaamua kuandika barua
inayosema "Samahani mume wangu, nimeamua
kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya
mbali na wewe"
Barua hiyo akaiweka juu ya meza iliyokuwa
chumbani.
Baadaye jioni, muda wa Mumewe kurudi
mwanamke huyo akajificha chini ya uvungu wa
kitanda mule chumbani
Mume alipoingia chumbani akakuta ile barua
juu ya meza, akaisoma kisha, akaandika
maneno fulani kwenye ile ile barua, harafu
akaanza kuimbaimba kwa furaha huku akipiga
miluzi na akiwa anavua nguo.
Akapiga simu na akasikika akisema hivi "hello
mpenzi, nina raha sana leo.. yule mwanamke
nuksi amesalenda mwenyewe kaondoka na
kutuachia uwanja, jiandae nakuja"
Muda huo huo Mume akaondoka.
Mwanamke alipokuwa uvunguni akawa anatoka
lakini amenyong'onyea na amelowa mashavu
kwa machozi.
Akasogea pale ilipo barua na akataka kujua
mumewe aliandika kitu gani kwenye ile barua.
Akakuta maneno haya "nimeona miguu yako
uvunguni, tafadhali andaa chakula nina njaa
sana mumeo, ila nimetoka kidogo nafuata
maziwa nilisahau kupitia. "

KAMEKUJA NA CHAJA YAKE

Jamaa aliona katoto kachanga kametoka kuzaliwa kakiwa bado
hakajakatwa kitovu akaropoka eti ,
"Hee ONENI, KAMEKUJA NA CHAJA YAKE"..

sikukuu ya wajinga

Mzee Shkamoo
Mzee mimi naitwa Jost, tunakaa Boko, zamani tulikuwa tunakaa Magomeni sasa baba alipopata hela za kustaafu akajenga huku Boko ndio tumehamia. Nimemamliza fom six niko nyumbani nangoja majibu. Kuna kitu naomba mnisaidie.
Tarehe 1 April nilimwambia baba yangu kuwa nimechaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Oxford Uingereza. Baba alifurahi sana akaagiza kuku wawili wachinjwe na mama apike pilau. Baada ya hapo kila siku amekuwa akirudi nyumbani kalewa anaimba kuwa mwanae ninaenda Uingereza. Juzi nimegundua kauza kipande cha ardhi jirani na kwetu ili aanze kukusanya fedha za mimi kuishi Uingereza. Pia nasikia ameshakopa hela Saccoss ili ajumlishe kwenye nauli yangu ya kuendea Ulaya. Pia alitoa shilingi laki tatu kanisani kama sadaka ya shukrani kwa mimi kuchaguliwa kwenda Uingereza. Mzee naomba unisaidie ntawezaje kumwambia baba kuwa siku ile nilikuwa namtania ilikuwa sikukuu ya wajinga?
Naomba msaada haraka au nitoroke kwetu?

Ohoo masikini umemezasoksi yangu

Siku ya harusi ilikuwa inakaribia,
lakini bwana harusi na bibi
harusi wote walikuwa natatizo
kubwa sana la siri, kila mmoja kichwa
kinamuuma itakuwaje ndoa
ikiianza. Bwana harusi akaenda kwa baba yake;
BWANA HARUSI: Baba ninatatizo nitafanyaje?
BABA: Tatizo gani mwanangu?
BWANA HARUSI: Baba nina
tatizo miguu yangu inanuka sana si mke
atanikimbia baada ya wiki
BABA: Uwe unaosha mara kwa mara harufu
itatoka
BWANA HARUSI:Baba hujui,harufu ni mbaya sana
BABA: Basi uwe unavaa soksi daima...jamaa
akaona hili linaweza
likanasaidia. Bibi harusi akaenda kwa mama yake;
BIHARUSI: Mama nina tatizo kubwa nikiamka
asubuhi mdomo
wangu unanuka mme atanikimbia
MAMA: Kila mtu akiamka asubuhi mdomo
unanuka hilo si tatizo.
BIHARUSI: Mama huelewi domo langu linanuka
unaweza
kufikiri panya kafa
MAMA: Basi ukiamka asubuhi usifungue mdomo
mpaka upige mswaki kwanza...
.Wapen zi hawa wakaoana na kila mmoja
akashilia ushauri mambo
yakawa powa.Siku moja baada ya miezi mitatu,
mume aliamka asubuhi
akagundua soksi moja imevuka, akahangaika
awahi
kuipata kabla mkewe hajaamka, bahati mbaya
mke akaamka;
MUME: Samahani umenionea
soksi?
MKE: Hapana,......ma ra harufu
mbaya ikaenea,
MUME: Ohoo masikini umemeza
soksi yangu.

MUNGU ANAKUONA

1. Unanunua gazeti la udaku halafu unaliweka
katikati ya gazeti la Mwananchi- Mungu
anakuona
2. Unajenga nyumba kisha unazungushia ukuta
wenye geti kubwa, kumbe ndani hakuna nafasi
hata ya kupaki baiskeli- Mungu anakuona
3. Home choo cha shimo, unadanganya eti
unatafuta fundi bomba flash imeharibika -
Mungu anakuona
4. Umekula ugali na bamia halaf unakuja
maskan na kijiti mdomon - Mungu anakuona
5. Unasoma karibunikutume secondary school
bt fb waandika unasoma feza- Mungu
anakuona
6. Kwa wale wanaoandika txt, 'Nakumiss'
halafu kuituma kwa wapenzi 20..........MUNGU
ANAWAONA
7. LUKU imekata kwenu umekaa nje unatext
watu,'Niko nje napata upepo
mwanana'.......MUNGU ANAWAONA
8. Huna kazi, mpenzi wako mtumishi wa serikali
mshahara laki 3 kwa mwezi, Birthday yako
unatumia milioni mbili......MUNGU ANAKUONA
9. We ni kiserengeti boy una mupenzi wa miaka
50, unamtext 'Njoo baby', we huyo baby au
nyanya yako?.....MUNGU ANAKUONA
10. Unapiga picha sebule ya boss wako
unaiweka FB na kukoment Home Sweet
Home........MUNGU ANAKUONA

Monday, May 19, 2014

Nataka kuruka

Jamaa mmoja alikua ana safiri kutoka kigoma kwenda DAR kwa treni walipofika katikati ya safari mambo yalikuwa hivi Jamaa- Nataka kuruka(maana yake ni kutapika kwa lugha ya waha) Abiria.-
jamani kamateni huyo anataka kuruka nje
Abiria wote walimshika kwa nguvu ili jamaa asijirushe nje baada yamda jamaa akatapika na kuchafua hewa ndani ya tren abiria wote walibaki na mshangao.