Rubani mmoja wa kigeni alikuja katika mbuga za Tanzania kwa
ajili ya uwindaji nyama pori.
Akawaajiri wawindaji wawili akawapeleka kwa ndege hadi
mbugani akawaacha wawinde ili akirudi na awachukue pamoja na nyama warudi
mjini.
Aliporudi baada ya wiki moja akakuta wamewinda nyama nyingi
kuliko uwezo wa ndege yake ndogo, rubani akaiangalia ile nyama kisha akawaambia
“hatuwezi kuibeba nyama yote hii pamoja na nyinyi ndege itazidiwa uzito,
itabidi nusu ya hiyo nyama tuiache”. Wawindaji wakasema “Mbona hata mwaka jana
pia tulibebe nyama nyingi kama hii, na sisi wa wili na rubani aliyetuajiri
katika ndege yenye uwezo kama wako, tuibebe tu”.
Rubani akasitasita lakini akaona awaamini akasema ” sawa
haina tatizo, kama mlibeba mwaka jana basi tubebe tu na mwaka huu”
Wakapakia nyama na wawindaji wakapanda kisha ndege
ikaondoka, ilipofikia katika mlima wakaribu ndege ikashindwa kuenda juu zaidi
kutokana na ule mzigo na hatimaye ikapata ajali katika mlima, kwa bahati nzuri
wote walipata majeraha tu hawakufa.
Rubani: (huku akiwa ajielewi kidogo) Hapa tulipoangukia ni
wapi?
Mwindaji mmoja: usijali, nahisi hapa ni karibu na pale
tulipoangukia mwaka jana