Katika kijiji cha Matare wilaya ya
Mugumu Serengeti, bwana
Wambura alikamatwa kwa kesi ya
kusingiziwa na kuhukumiwa kwenda
jela miaka mitatu.
Huku nyuma akiacha mke na
watoto wanne waliokuwa
wanasoma. Hukumu hiyo ilimtesa
sana kichwa chake, alitamani kila
mtu anayemhisi kuwa ana makosa
aingie katika moyo wake na
kuupata ukweli.
Alilia na umaskini wake, lambda
angepata wakili mzuri angeweza
kumtetea, kumkosa wakili
kukahalalisha kifungo hicho!!
Alikwenda gerezani huku akiumia
sana rohoni. Aliyaanza maisha
mapya kwa shida sana, akawa
mnyonge kila mara na mwili
ukapoteza afya kiujumla.
Huko gerezani alifanikiwa kupata
rafiki aliyekuwa na cheo ama
jukumu la uzikaji wa wafungwa
hasahasa ambao hawakuwa na
ndugu ama ambao ndugu zao huwa
hawajitokezi pale gerezani.
Mzikaji alijaribu sana kumtia nguvu
Wambura na kumwaminisha kuwa
hiyo ilikuwa hatua tu ya maisha
anapaswa kuizoea na siku moja
ukweli utajulikana tu! Bwana
Wambura maneno ya mzikaji
hayakumuingia kabisa.. alizidi
kunyong'onyea.
"Siwezi kuvumilia kukaa gerezani
miaka mitatu…..kama unajali kilio
changu nisaidie nitoroke kwa
namna yoyote ile ndugu yangu!!"
Wambura alimsihi mzikaji.
SIKU MOJA mzikaji akamwambia
Wambura kuwa msaada
umepatikana. Lakini yataka moyo!!
"Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu
nitoke humu!!" alijibu kwa msisitizo
huku akimtegea sikio mzikaji.
"Msaada pekee wa kukutorosha
humu ndani ni kwa njia ya jeneza…
yaani mfungwa akifa mimi
nakuunganisha naye kwenye
jenerza….." akashusha pumzi kisha
akaendelea "Wewe ukisikia kengere
ya msiba, njoo mara moja kwenye
chumba cha maiti, utakuta tayari
sanduku liko katikati ya chumba
linakuwa halijafungwa, funua
kifunioko ingia ndani yake ulale
pembeni ya maiti kwani sanduku
huwa kubwa la kutosha kila aina ya
maiti na hata miili miwili inaingia.
Kisha nitakuja na kulipigilia
misumari. Baada ya mudap
tutalipakia kwenye gari na kutoka
kwenda nje ya gereza makaburini
nikiongozana na baadhi ya
wafungwa na maaskari magereza.
Tutakuzika huko lakini baada ya
dakika 20 hadi 30 nitarudi
kukufukua. Hautaweza kushindwa
kupumua kwa dakika hizo, utatoka
ukiwa huru."
JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini
lilimtisha sana Wambura. Hata
hivyo akaona afadhali afanye hivyo
kuliko kukaa gerezani miaka mitatu
bila kosa.
Siku moja akasikia kengele ya
msiba. Akafanya kama
alivyoelekezwa na mzikaji. Akaenda
na kuingia chumba cha maiti. Kweli
akalikuta sanduku, akiwa na hofu
kuu akaingia na kulala pembeni ya
maiti iliyokuwepo. Mara akasikia
mtu ameingia na kulipigilia
msumari sanduku. Muda mfupi
baadaye sanduku likainuliwa na
kuwekwa kwenye gari.
Gari ikatoka nje ya gereza hadi
makaburini. Sanduku likashushwa
na kuwekwa kaburini na kuanza
kufukiwa.
Wambura alijitahidi sana kuvumilia
japo hofu ilizidi kutanda.
Alimtegemea sana mzikaji na
alianza kumuona mkombozi wa
maisha yake.
Kama alivyoambiwa, akasubiri
dakika kumi, ishirini.. zikapita
kimya!!
Dakika thelathini kimya. Joto nalo
likazidi kuongezeka.
"Nitavumilia hadi afike…"
alijisemea kisha akajiongezea kauli
ya ujasiri.
"Kama nilitakiwa kuishi gerezani
miaka mitatu kivipi dakika kadhaa
za hapa kaburini"
KWA kuwa alishakaa gerezani kwa
muda kiasi akatamani kujua
aliyekufa ni nani… ni kwewli
aliogopa kuitazama maiti lakini
aliona kama inatisha zaidi ikiwa
imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi.
Akaifunua upande wa usoni… Kwa
kuwa kulikuwa na giza nene
alikodoa sana macho kuitazama.
LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA
NA SURA YA MZIKAJI!!!