tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Tuesday, May 20, 2014

hali ya baba nayo siku hizi si nzuri sana

Familia moja ilishangazwa pale
walipopokea jeneza la marehemu mama yao


aliyefariki nchini Marekani. Lilitumwa na mmoja ya watoto wake wa kike.

Mwili ndani ya jeneza ulikuwa umesongwa sana
ndani ya jeneza kiasi

kwamba uso wa marehemu ulikuwa umegusa kioo cha jeneza!

Walipofungua jeneza, walikuta barua juu ya merehemu, iliyosomeka namna

hii:

'Wapendwa ndugu zangu, nimeutuma mwili wa mama yetu kwa ajili ya

mazishi, kwani imekuwa siku zote hamu yake kubwa kuzikwa nyumbani Machame,
katika nyumba ya ukoo. Samahani sikuweza kuja na mwili kwani

nimenyimwa likizo kwani kuna upungufu wa wafanyakazi hapa kazini mwezi

huu.

Ndani ya jeneza, chini ya mwili wa mama, kuna makopo 12 ya samaki wa

makopo, paketi 10 za supu ya Royco na chupa 8 za jam ya maembe. Mgawane

hivi kwa jinsi mtakavyoamua nyinyi.

Katika miguu ya mama kuna pea moja ya viatu vya Reebok namba 9 kwa ajili

ya mtoto mkubwa wa Mushi. Pia, kuna pea mbili za viatu kwa ajili ya

watoto wa Urassa na Kwayu, natumaini nitakuwa sijakosea namba za miguu.

Nimemvalisha pia mama American T-shirts 6, kubwa kabisa ni kwa ajili ya

Manka, na zinazobaki ni za watoto wake. Hizo jeans mpya 2 ambazo mama

amezivaa ni za wavulana. Hiyo Swiss watch mkono wake wa kushoto ni

zawadi ya Koku kwa ajili ya sikukuu yake ya kutimiza miaka 21. Anti

Rebeka, hizo heleni, mkufu na pete ambazo mama amevaa ni zako.

Hizo soksi 6 ambazo mama amevaa wagaiwe wajomba. Tafadhali mgawane kama

nilivyosema na kama kuna kitu kingine mnahitaji, basi mnieleze kwani

hali ya baba nayo siku hizi si nzuri sana.

Dada yenu mpenzi,

Mama Manka