Padre mmoja mzee alistaafu na wanaparokia walimfanyia
sherehe kubwa. Katikasherehe hiyo, mbunge wa eneo hilo alipangwa kutoa hotuba
ya shukurani yakumuaga padri huyo kwa niaba ya wanaparokia wote. Bahati mbaya,
mbungealichelewa kufika ....
Mc akamwomba padri aseme machache wakati wanamsubiri
mheshimiwa mbunge.
Padri hakujipanga kusema kitu lakini kwa kujitahidi,
aliongea.
"Wapendwa, naikumbuka sana siku nilipofika katika
kanisa hili kwa mara yakwanza, ila nilipata mshangao siku nilipoanza
kuungamisha. Mtu wa kwanzakabisa kumuungamisha alinishangaza sana. kwani
alisema amemwibia bosi wakeTV, amemwibia ndugu yake pesa za urithi, amezini na
jirani yake, na piakatembea na house girl wake. Nikapata picha kuwa kumbe watu
wa kanisa hilindivyo walivyo, nikasikitika sana. Kumbe nilifikiria tofauti.
Kwani baadayenikakuta kumbe watu wa hapa ni wazuri sana na hawatendi dhambi
mara kwa marana ni wastaarabu sana".
Mara mheshimiwa mbunge akawasili, padri akakatisha maongezi
na mbungeakaanza kuhutubia. "Ndugu wapendwa, naomba mniwie radhi kwa
kuchelewa kwaninilikuwa na majukumu makubwa ya kiserikali. Pia ninayo furaha
kubwa kwakunipa nafasi hii kuhutubia kwa niaba yenu. Mimi nina bahati sana
kwani padri huyu alipokuja hapa, mimi nilikuwa mtu wa kwanza kwenda na kuungama
kwake....