tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Sunday, June 2, 2013

nakutumia kiss 100

Jamaa alihamia Dar tokea Mbeya kwenda kusaka life na kumwahidi wife kuwa atakuwa akimtumia fedha za mahitaji ya yeye na familia, sasa jamaaa akiwa Dar mammbo yakawa sioikabidi amtumie wife barua na kusomekahivi:-

Mpendwa mama wa watoto wangu,

Ni matumaini yangu kuwa u mzima wa afya pamoja na wanangu wote.

Hapa dar hali imekuwa ngumu na nimeshindwa kukutumia fedha za matumizi ya mwezi ila nakutumia kiss 100 kwani nakupenda sana.
Salimia familia kwaniaba yangu.

Mmeo mpenzi

Baada ya wiki mbili jamaa nae akapokea barua toka kwa mkewe ikisomeka kama ifuatavyo:-

Mme wangu mpenzi,

Kwanza pole na mihangaiko na hali ngumu uliyonanyo.

Kuhusu fedha usijali kwani nimezitumia zile kiss 100 ulizonitumia na ufuatao ni mgawanyo wake

1. Baba mwenye nyumba alivyokuja kudai kodi ya nyumba nilimalizana nae kwa kiss 35

2. Na Yule mangi wa pale dukani ambaye alikuwa ananidai fedha za baadhi ya majitaji ya nyumbani nimemlipa kiss 10

3. Maji na umeme walivyokuja kunidai nimewapa kiss 20

4. Mwalimu wa tution yeye amekubali kwa kiss 25

Usijali sana kwani mpaka sasa nimebakiwa na akiba ya kiss 10.

Nakutakia kazi njema na mafanikio

Mkeo kipenzi
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania