tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Saturday, October 12, 2013

Wanaume walikuwa kwenye semina

Wanaume walikuwa kwenye semina wakaulizwa.
Mara ya mwisho kumwambia mkeo unampenda
ni lini? Wengine wakasema leo asubuhi,wengine
muda sio mrefu. Muwezeshaji akawaambia kila
mmoja sasa hivi amuandikie mkewe sms
amwambie nakupenda mke wangu halafu
badilishaneni simu kila mmoja asome majibu ya
mwenzake.Majibu yalikuwa hivi:-
1.Unaota au?
2.Umekumbwa na nini?
3.he, Makubwa!
4.Utanieleza hii sms ulikuwa unamtumia nani!
5.Leo sikusamehi najua kuna kitu.
6.Huyo ulienae ndo kakwambia unitumie hii
sms?
7.Najua tu tayari kuna kitu umeharibu.
8.Wewe sema unacho kitaka.
9.Leo hunipati ng'o!
10.Nani mwenzangu?