tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Saturday, October 12, 2013

KUNA WIZI UMETOKEA BENKI

Jambazi "wote laleni chini pesa ni za serikali na maisha ni ya kwenu", wote wakalala chini
HII INAITWA DHANA YA USHAWISHI - kubadilisha njia ya kawaida ya kufikiria
••••••••••••••••••••••
Kuna dada kwa woga akawa amelala chini kimitego, Jambazi akamwambia, "dada hebu kuwa na adabu chukua kanga jifunike hili ni tukio la ujambazi na sio la ubakaji."
HUU UNAITWA WELEDI - zingatia ulichofundishwakufanya
•••••••••••••••••••••••
Walipotoka kwenye wizi jambazi mdogo ambaye ana shahada ya uzamili ya biashara akamwambia mwenzake, "tuzihesabu hizi fedha." Yule mkubwa akamcheka kwa dharau na kumjibu, "wewe mjinga sana hizo hazina haja ya kuhesabu saa mbili watatutangazia kwenye taarifa ya habari tumeiba kiasi gani.
HUU INAITWA UJUZI - Siku hizi ujuzi ndio bora kuliko vyeti
•••••••••••••••••••••••
Baada ya majambazi kuondoka meneja akamwambia mhasibu wa bank, " ujumlishie na zile milioni 80 tulizo iba sisi."
HUKU KUNAITWA KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI - kushabihiana na mazingira magumu kwa faida binafsi.
•••••••••••••••••••••••
Mhasibu akafurahi na kusema, "dah wizi ukitokea kila mwezi itakuwa burudani sana."
HUKU KUNAITWA KUWA NA MAWAZO CHANYA - Furaha ndio kitu cha muhimu zaidi
•••••••••••••••••••••••
Meneja kafurahi sana kwa kuwa sasa matatizo yake yametatuliwa na wizi uliojitokeza.
HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU- shikilia nafasi pale inapojitokeza hata kama ni hatari kiasi gani.
•••••••••••••••••••••••
Haya usiku wake taarifa ya habari ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana wa million 100 umetokea leo benki. Majambazi kuskia hivyo wakaanza kuhesabu zile pesa lakini wakajikuta na milioni 20 tu. Yule jambazi mkubwa akashtuka na kusema, "dah! yaani meneja kaiba mara nne zaidi yetu bila kuchezesha msuli? Bora umeneja kuliko ujambazi."
HII INAITWA ELIMU NDIYO KILA KITU - ishike sana elimu ina nguvu kuliko dhahabu
•••••••••••••••••••••••••••••