tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Friday, September 9, 2016

STRESS NI NINI

Stress ni pale unapompa msichana lift halafu akazimia ndani ya gari yako na humjui wala hujui kwao. Ulimkuta tu njiani ukamsaidia.!

Noma zaidi ni pale unapoamua kumpeleka huyo msichana hospitali na akabainika ana mimba dokta akaanza kukupongeza kuwa unakaribia kuitwa baba!

Stress ya tatu ni pale unapokataa na kumwambia dokta mimba si ya kwako, mara ghafla msichana anazinduka na kudai mimba ni ya kwako?

Stress ya nne ni pale dokta anapoamua kukupima ili kuthibitisha, na baada ya vipimo anakwambia mimba si yako kwakuwa huna uwezo wa kumpa mwanamke mimba.!

Stress ya mwisho ni pale,, unaporidhika majibu ya doctor kuwa huna uwezo wa kumpa mwanamke mimba lakini unakumbuka nyumbani una mke na watoto wawili.....!!!!!!