tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Thursday, September 29, 2016

Nyoka

umerud geto mida ya saa mbil ucku unaingia ndan ghafla unamuona nyoka kanyanyua shngo juu ana chzesha mkia na ki ulimi kinatoka toka nje.....Kwa ujasili unaamua kuchukua fmbo ili kumuua ...lkn ulivo jasiri zaid unaamua kufnga na mlango af funguo unatupia ktndan unajarbu kumdhuru lkn ghafla umeme unakatika
Hapo ndo utajua nobody can stop Reggae

Wednesday, September 28, 2016

Daladala

Nimepanda daladala inavuja mpaka nikamshauri dereva aache kubeba abiria alime mchicha, hatuwezi kulowa hivi kwa daladala.

Sipendi uzembe mimi

Friday, September 23, 2016

Mwizi

Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu
akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid
na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae
maana hta hela ya kula Jana sikua
nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu?
sipendagi utani na kitu hela mm!

Nani aliuwa Goliath

WAZAZI PELEKENI WATOTO SUNDAY SCHOOL PLEASE!!

TEACHER: Nani aliuwa Goliath......
STUDENT 1: Sio mimi.
STUDENT 2: Sikuwa shule jana. .
STUDENT 3: Mimi sijui.

(The Teacher went and told the Headmaster ati watoto wa hio class hawajui nani aliuwa Goliath.) ... ( headteacher goes to the class.)

HEADTEACHER: Nani aliuwa Goliath.
CLASS: Sio sisi.
H.TEACHER: Mkikosa kuniambia hii darasa itawaka moto.
CLASS: Hatujui teacher.

The H.TEACHER turns and asks the teacher....

"Uko sure Goliath aliuliwa na mtu wa hii
darasa?"

The teacher fainted...

Wednesday, September 21, 2016

Mke wangu

ETI NAMTONGOZA DEMU NAMPA NAMBA ALAFU ANAMPA BOYFRIEND WAKE AKANIPIGIA WE NANI UNAMTONGOZA MKE WANGU NIKAMJIBU MI MUHUDUMU WA GEST MWAMBIE AMESAHAU CHENCHI

Nimekunja sura

Leo kuna mtu nimemtolea uvivu ! amenikuta nimetulia akaniuliza mbona nimekunja sura ...nikamwambia nataka kuiweka kwenye bag.

Sipendangi ujinga mimi

Nilikula kuku

Unamualika binti luch harafu anakuja na maringo, eti oooh.....! Bebe ata sitakula wakati natoka home nilikula kuku....!!

Wewe kwa ugetlemen wako unamnunulia Whisky ya Jack Daniels ya elfu hamsini!

Baada ya binti wa watu kunywa mafunda kadhaa anatapika makande na mahindi ya kuchoma wallah...!!

Sasa apo inabidi umulize romantically .....!!

Sory baby...! Uko sure ulikula kuku au chakula cha kuku

Monday, September 19, 2016

Simu

Siku moja mfanyakazi alienda ofisini uku masikio
yake yote mawili yakiwa yamefungwa bandeji.
Bosi wake akamuuliza imekuaje kuhusu masikio
yako?. Jamaa akajibu.
"jana wakati napiga pasi nguo zangu, simu iliita, kwa
bahati mbaya badala ya kuweka simu sikioni nikaweka pasi".
"Sawa" Bosi akasema, "iyo ni kuhusu sikio moja, na
ilo sikio lingine ilikuaje?" Jamaa akajibu
"simu iliita tena!"

Wazazi wako

Unakutana na mdada ndani ya miezi miwili anataka aje waona wazazi wako. Dada, mi mwenyewe nlikaa miezi 9 tumboni kabla sijawaona wazazi wangu mwenyewe, usiniletee mapenzi ya Mwendokasi.

Sipendagi ujinga mimi

Nyumba za kupanga

UTAMU WA NYUMBA ZA KUPANGA!
Jana neighbor yangu alikuja
akaniambia nipunguze sauti ya radio
anataka kulala.
Leo anapika chapat na mimi
nmemwambia apunguze harufu ya
chapati nataka kula ugali. sipendi ujinga ajue.

Sunday, September 18, 2016

Vipofu

Jion ya jana niliwakuta  vipofu wawili wakipigana
Basi nikapaza sauti na kusema ninamsapoti huyo aliye na kisu
Ghafla wote wakaanza kukimbia mmoja kule mwingne huko.
Ila hakuna aliyekuwa na  kisu

Huwa sipendagi ugomvi mimi

Malaika

MTOTO: mama kwa nn unamuita mdogo angu malaika
MAMA: kwa sababu yeye ni mdogo sana na yupo kama malaika,
kwa nini umeuliza mwanangu?
MTOTO: nimemrusha dirishani nashangaa hajapaa

mama kazimia!!!

Friday, September 16, 2016

Mkopo

Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.

Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!

Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsApp...!

Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang'oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri.

Kisha nikaituma ile message

Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yake... Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.

Akatuma message akiniuliza...

Hao wanawake unawajuwa, ...mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweli...!

Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaa...!

Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaa...! Akaniandikia message nyingine....

...Nakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupe... Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuri...!

Nami nikamjibu...

Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipo...!

Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdai...!

Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaa.... Kama sio mie!

Wednesday, September 14, 2016

Daladala

Watu wengine bhanaa!!

Jana nilipanda daladala basi ile kaka yenu nikawa nimejiachia kuchati, kuna jamaa akawa anasoma msg zangu bila aibu yani anafutilia ninavyochati...

Basi nikasema ngoja nimtie Adabu.. Nikaamua nimtext jamaa "Oya Alex ngoja nilipue hii daladala muda ushafika" Yule jamaa akajirusha dirishani......
Na kavunjika miguu na kiuno........

Sipendi mambo ya kijinga mimi

Tuesday, September 13, 2016

Mwanamke

...ingekuwa vp dunia ingeongozwa na mwanamke kungekuwa hakuna vita, ungesikia tu.. Marekani aiongei na urusi, mara rwanda yainunia burundi, boko haramu yawapelekea umbea alshabaab, ethiopia yasusia misaada ya UN, mara djibout yamtuma balozi wake kuisuta sudan, waziri mkuu wa UK awachambe magaidi wa qt.. Yaani ingekuwa amani tu..!!
#shikamooni_wanawake

Friji

WABONGO KWELI MTIHANI
SINA HAMU NAO...!!

Jamaa alinunua friji jipya, akawaza namna ya kuondokana na lile la zamani, basi akaliweka nje ya nyumba yake na kuandika kibao:

"ANAYE TAKA KUCHUKUA, ACHUKUE BURE"

Watu wakawa wanapita wanafungua lakini kila mtu akawa anaogopa kuchukua maana hakuna aliyeamini mtu anaweza akagawa friji zima bure.

Baada ya kuona wiki imepita halijachukuliwa, akahamua kubadilisha kibao na kuandika:

FRIJI LINAUZWA SHILINGI LAKI MBILI NA NUSU TU

Usiku ule ule likaibwa

Sunday, September 11, 2016

Mkopo wa Chuo

Wenzako wanapokea mshahara M3 kila mwezi na bado wako single,wewe unapokea mkopo wa chuo unatuambia unataka kuoa....!!
Ulitakiwa upigwe KOFI la kichwa tu restore settings.
#PumbavuKabisa

Friday, September 9, 2016

STRESS NI NINI

Stress ni pale unapompa msichana lift halafu akazimia ndani ya gari yako na humjui wala hujui kwao. Ulimkuta tu njiani ukamsaidia.!

Noma zaidi ni pale unapoamua kumpeleka huyo msichana hospitali na akabainika ana mimba dokta akaanza kukupongeza kuwa unakaribia kuitwa baba!

Stress ya tatu ni pale unapokataa na kumwambia dokta mimba si ya kwako, mara ghafla msichana anazinduka na kudai mimba ni ya kwako?

Stress ya nne ni pale dokta anapoamua kukupima ili kuthibitisha, na baada ya vipimo anakwambia mimba si yako kwakuwa huna uwezo wa kumpa mwanamke mimba.!

Stress ya mwisho ni pale,, unaporidhika majibu ya doctor kuwa huna uwezo wa kumpa mwanamke mimba lakini unakumbuka nyumbani una mke na watoto wawili.....!!!!!!

Mtangazaji

Nimejisikia furaha sana leo nimewasha Redio nkasikia Mtangazaji wa KIKE  ananambia "MPENZI MSIKILIZAJI NAKUPENDA SANA ENDELEA KUWA NA MIMI KTK KIPINDI CHANGU"!!
Nimefurahi sana ila bado cjampa jibu kama na mimi nampenda au la!!

Demu

Umexhawah kuwa single had ukaamua kununua viatu vya kike kixha ukaviweka mlangon ili majiran wakipita wajue una demu ndani...

KUA SINGLE NAO NI UGONJWA EEENH

Mbuzi wa IDD

Family walinunua mbuzi wa IDD kabla kwa miezi miwilli.
Mbuzi akawazoea sana hio family na akawa anakula nao na kulala nao.
Siku ya IDD ilipokaribia mbuzi aliingia nyumbani huku machozi yanamtoka
Akaulizwa kwa nini unalia?
Akasema majirani wote wamenunua mbuzi wa IDD isipokuwa sisi.

Mhudumu

Leo nilienda kula hotelin nikamkuta ex wangu analumbana na wahudum kumbe kala kashindwa kulipa ikabidi wampeleke jikoni akasaidie kumenya viazi ili wamsamehe deni! Asee ilinigusa mnoo nikamwita yule mhudumu nikampa hela wanunue gunia jingine la viazi

Kang'atwa na nyoka

mdada:-    Bby naomba hela nimpeleke mdogo wangu hospital kang'atwa na nyoka
JAmaa:- embu mpe huyo nyoka simu niongee nae..
maisha yanakaba..

Hoteli

Kuna demU ameangusha kipochi leo, nikamwambia "Excuse me madam" akasema "I have a boyfriend" saa hii niko kwa hoteli nakula kuku••

#Maringo_sipendangi..

Salon

DADA alienda Salon wakati anasukwa akaingia MKAKA mtanashati, DADA akaamua kujaribu bahati yake.
DADA:Mambo?
KAKA:Poa.
DADA:Mimi na wewe tunaweza kuongea baade?
KAKA:Kuhusu nini?
DADA:Nimekupenda nataka nikutoe out.
KAKA:Sawa ila nitamwambia nini MKE wangu?
DADA:Aah ilo sio tatizo mdanganye tu,mwambie unakwenda kumtembelea rafiki yako hospitalini.
KAKA:Mwambie mwenyewe huyo hapo anayekusuka.Unajua nn kiliendelea?
Subiri ni chaji cm.

Thursday, September 8, 2016

Wanawake banaa..

Akikuta Pesa kwenye suruali wakati Wa kufua hata hasemii inaondoka kimya kimya   ..ila akute kondom sasa izo kelele zake utajuaa kama ulioa mwanamke au kipaza sauti
Kutoka mahali.

Mungu anawaona

Sunday, September 4, 2016

Panya

Nimeingia chumban  nikakuta panya wamekula dawa yangu ya menoo, Na mimi nimechukua yakwao nikanywa. Sipendagi ujinga mimi

Mwanafunzi

Unamtongoza mdada anakujibu et "bado nasoma" Dada kwani nimesema ukinikubalia ntakuchania Madaftari?