tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Monday, March 28, 2011

akija na mananasi

Jamaa watatu walikuwa wakisafiri kupitia kwenye msitu mnene na kwa bahati mbaya wakakutana na majitu yanayokula watu na yakawakamata. Yale majitu yakawaambia 'sisi tuna mtihani ambao ukifaulu tunakuacha uende zako, la ukishindwa unaliwa.'

Basi yale majitu yakawatuma msituni wakiwa chini ya ulinzi kukusanya kila mmoja wao matunda kumi ya mti watakaochagua.

Baada ya muda mfupi mmoja wao akawa amefanikiwa kurudi na matunda aina ya Apple. Akaambiwa mtihani mlionao ni kuhakikisha kuwa unakula matunda yote kumi kwa kumeza bila kutafuna, moja moja lakini usionyeshe hisia yeyote katika uso wako.

Yule aliyekuja na apple akaogopa mno lakini akajizuia kuonyesha hofu yake, wakati huo huo yule wa pili akawa anakuja na matunda yake mkononi aina ya rasberry ambayo ni madogo na hayana kokwa. Yule wa kwanza alipoweka apple mdomoni kwake lilimzidi kinywa na hivyo akagugumia maumivu kwa hiyo akaliwa mara moja.

Huyu wa pili kuona hivyo akazuia hisia zake za hofu kubwa na akapewa mtihani ule ule wa kula matunda hayo moja baada ya jingine. Kutokana na udogo wa matunda hayo na kuwa hayana kokwa ndani alikula bila matatizo mpaka tunda la tisa.

Alipofika tunda la tisa akaangua kicheko kikubwa mno kwa ghafla hivyo na yeye akaliwa mara moja.

Mara wakajikuta wako ahera yule wa kwanza na wa pili. Yule wa wa kwanza akashangaa sana na kumuuliza 'imekuwaje wewe umeshindwa kula vile vijitunda?' Huyu wa pili akajibu na kusema ' nilimwona jamaa yetu wa tatu akija na mananasi'