tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Saturday, September 11, 2010

Wachaga

Wamachame, wako very carefull.

Ukijipendekeza kwa binti wa huko, Yahye, uchumba tu, lazima upeleke kapppatti la mbeho!

Wakibosho (Specialized banits)

Yao kali, mama akiwa anapiga soga na mwenziwe utamsikia anavyomsifu mwanawe kama hivi. “Eee dada; Yaani dadangu, we acha tu Yule Alex wangu siku hizi amepefuka  kweli; ameendelea kweli. Ana akili we acha tu’ haibi tena mifukoni siku hisi, ameunda kundi lake la ujambasi. Krisimasi hii lasima nitaletewa fitenge file fya kongo.
Kivumbi ni pale Binti akiolewa na kyasaka (mtu ambaye sio mchaga) wazazi wake baba na mama wanamwambia “hivi we huyo mwanaume kwani ni ndugu yako? Leta hizo pesa zake tujenge huku kwetu Manka”

Wauru

Nao wanachosha kweli, wakikakaa ni kuongea kuhusu shule tuuuuuuuuuuuu, masomo, digrii. Yaani yu  ‘kanot bilivu’ babu wa miaka 70 bado madafutari yake ya primary ameweka sandukuni!! Atawaonyesha wajukuu zake wote: “ona hand writing yangu ilivyokuwa nzuri wakati nafundishwa na Father Wilson Payatt.” Wanakumbuka majina ya walimu wao hasa wazungu tangu chekechea. Uzuri wao wanamuogopa sana Mungu. Kengele ya kanisani saa sita mchana utaona wazee wote kilabuni wanaamka na kusali sala ya mchana ndio wanaendelea kunywa mbege yao. We acha tu.

Wale wa Old Moshi (The Mechanics)

Wanawake wana haki ya kuringa. Ni wazuri kweli kweli, yaani mi sisemi we nenda utajionea mwenyewe. Tabu ni kwa wanaume ni wabishi kama mkia wa mbuzi, wanakunywa kisusio hata cha Nguruwe na Gongo nyingiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii (wenyewe wanaiita Crysta-pen)
Wao pia kama dada zao ni (the handsome) chunga mkeo asiwazoee wana visu vikali na hupenda pia nyama choma.