tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Thursday, March 17, 2016

Mkulima

Mkulima Jipu......

MWANDISHI: Wewe unawalisha ng'ombe chakula gani?,
MKULIMA: Ng'ombe yupi Mweupe au Mwekundu?
MWANDISHI: Ng'ombe mweupe
MKULIMA: Ninamlisha nyasi na viguta vya mahindi,
MWANDISHI: Na mwekundu??
MKULIMA: vilevile nyasi na viguta vya mahindi,
MWANDISHI: ahaa sawa,na sehemu ya kulala ni wapi?
MKULIMA: Ng'ombe yupi mweupe au mwekundu?
MWANDISHI: Mweupeee!!!
MKULIMA: Mweupe ninamlaza bomani kulee,
MWANDISHI: na mwekundu?
MKULIMA: vilevile ninamlaza na mwenziwe!!!!
MWANDISHI: Hii sehemu yote majumba mengi, wakienda kulisha unafanyaje?
MKULIMA: Yupi mweupe au mwekundu?
MWANDISHI: Woteee!!!! {kwa hasira}
MKULIMA: Mweupe nina mfunga kamba na kumzungusha malishoni na kumrudisha,
MWANDISHI: na mwekundu vilevile?
MKULIMA: Mwekundu?, mwekundu ninamfunga
kamba na kuzunguka nae kama mwenziwe!!!
MWANDISHI: Kwanini kila mara nikikuuliza huduma za ng'ombe zako unaniuliza mweupe
au mwekundu halafu inatokea kuwa kazi zao wote ni sawa??,
MKULIMA: Kwasababu Ng'ombe mweupe ni wangu,
MWANDISHI: Na mwekundu?
MKULIMA: Ni wangu vilevile!!!!!