tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Friday, March 18, 2016

Mama mkwe

Mama mkwe kamkuta mkwe (mume wa bintiye) sebuleni akiwa kafura na kapandisha hasira anadai ataua mtu.

Mama Mkwe: Mwanangu kwani kuna nini jamani?
Jamaa: Leo namuua mwanao, mshenzi sana.
Mama Mkwe: Tulia jamani, kimetokea nini?
Jamaa: Mwanao mshenzi sana, nilikuwa nimesafiri, nikamtumia meseji kuwa nakuja, eti bado leo nimefika nimemkuta na mwanaume kwenye kitanda chetu, dharau gani hii, sikubali leo tunagawana majengo ya serikali, yeye anaenda kulala Muhimbili mi naenda kulala Segerea
Mama Mkwe: Subiri kwanza, mwanangu hayuko hivyo lazima kuna maelezo fulani kuhusu hili ngoja nimuulize...mama mkwe akamfwata mwanawe na baada ya muda akarudi sebuleni.
Mama Mkwe: Unaona, nilijua mimi lazima kuna sababu. Kumbe mwenzio hakupata ile meseji uliyomtumia.