tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Sunday, March 13, 2016

Maisha yamenishinda

Jamaa kamkuta mwanamke mmoja pale Ferry analia,

JAMAA: Nini shida mama angu?

MDADA:Heri nife, maisha yamenishinda

MJAMAA: Huna haja ya kufa, sikiliza mimi ni baharia na meli yetu inaenda Ulaya leo, kama unataka ingia kwenye boksi nikakufiche stoo, meli ikitia nanga Ugiriki, nakutoa ukatafute maisha huko. Bibie akaona heri hilo akaingia kwenye boksi, jamaa akambeba na mdada akajikuta yuko kwenye stoo moja wapo katika meli, jamaa akawa anamletea chakula kila siku na mara nyingine yeye mwenyewe analala huko kwenye hako kastoo kama binadamu wengine walio kamilika walikuwa wanafanya na ya kwao huko huko kwahyo safari ilikuwa nzuri hasa kwa jamaa, kila mara akimhakikishia mdada kuwa wameshapita visiwa vya Komoro, siku nyingine akimwambia wako India. Zilipita wiki mbili ndipo yule mdada akagundulika na nahodha wa chombo hicho.

NAHODHA:We unafanya nini humu?

MDADA:Chonde naomba msinitupe baharini, nilindeni mkifika Ugiriki mnishushe

NAHODHA: Unajua mbona sikuelewi? Mdada akalazimika kumueleza nahodha ishu nzima.

NAHODHA:Dah wala usipate taabu sikutupi popote, ila jamaa yako kakudanganya hii si meli ya kwenda Ulaya ni pantoni ya kwenda Kigamboni, umekuwa unazunguka hapa hapa Dar siku zote hizo, haya tukifika Kigamboni  shuka...