tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Thursday, October 21, 2010

Mambo ya ajabu

Mambo yanayokera na kusababisha uonekane ovyo. Unamwita mtu usiyemjua  (wala kukutana naye kabla) aunt au uncle ama shemeji. Wizi mtupu.
Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao ambao gharama za  kupiga simu ni nafuu (mfano usiku sana) na mara nyingi  huwa una beep tu.
Asilimia 90 ya DVD pamoja na CD za muziki ulizonazo nyumbani ni feki (sio original copies) na hata original copies ulizonazo umeazima na haurudishi mpaka mwenyewe aje kuzifuata.
Stoo yako imejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi. Acha hizo!
Una machupa ya maji matupu ya shampoo perfume pamoja na vipozi vingine umeweka tu wala huna shughuli navyo.
Watoto wako wote wana majina utani mfano babu Ali, Chidi, Mamu, Dida, Kadogo, Asha ngedere, dada Kiboga n.k
Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno, tissue ulivyochukua sehemu kama vile hotelini.