tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Thursday, October 7, 2010

jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha basi wakafanya mazungumzo. 
Mmoja aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake hatimaye mwenzake 
akasema " Unadhani familia yako ina matatizo?" Basi sikiliza kisa hiki. 

" Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti 

mkubwa tu na tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu 

wa kambo hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na 

Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu 

akawa mama mkwe wa mkwe wake. 

Baadaye binti yamke wangu yaani binti yangu wa kambo alipata mtoto wa

kiume. mtoto huyo wa kiume alikua ndugu yangu kwa sababu tulichangia 

baba mmoja. lakini kwa vile alikua ni mtoto wabinti wa mke wangu papo hapo 

akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake mdogo wangu. 

Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto 

wa kiume. Sasa msichana ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume 

kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia 

baba yangu kua shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa 

upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji 

yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) 

wabinti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu 

ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe.