tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Sunday, April 17, 2016

Mmeo

Kuna Jamaa Kwenye Daladala Hapa Alikuwa Anaongea Na Simu....... Halooo Leo Sitaweza Kuja Nimepanda Gari Moja Na Mmeo...... Unaambiwa Wanaume Wote wenye Wake.... Wamemng'ang'ania Aoneshe Hiyo Namba Aliyokuwa Anaongea Nayo...... Sijui Kamalizana Nao Vipi Maana Mimi Nilishuka Kituo Kilichofuata.

Friday, April 8, 2016

Faraja

Ukikaa ukitafakari kuna milio mingi saana duniani ya gitaa,kinanda,pikipiki,gari etc.....lakini ule mlio m1 wakati ATM inatoa fedha ule grrrrr grrrr hua una faraja saana moyoni.... Daah pesa huyu

Wednesday, April 6, 2016

Unywaji pombe

Chukua tahadhari,

Unywaji pombe kupita kiasi hupelekea upungufu wa kumbukumbu na matatizo mengine mengine......... ambayo siyakumbuki vizuri!

Bahati iliyoje

BAHATI ILIOJE HII JAMANI.
××××××××××××××××××

Kuna siku nilikuwa maeneo ya Mjini kati
(City Center), nikaipenda suruali moja ya
shilingi 15,000/= na pesa sikuwa nayo
ikabidi niende kutoa kwenye ATM ya
Postal.
Nimefika pale sikukuta mtu hivyo
niliingia moja kwa moja, nimefika mle
ndani nikakuta Pesa Kibao zimemwagika
pale kwenye kitundu cha kutolea pesa,
ATM Card ilikuwepo pale imetokezea na
Pembeni kulikuwa na Pochi ya Kike
iliyoonekana kutuna vilivyo.
Kwa woga mimi huku nikitetemeka
mapigo ya moyo yakiwa yameongezeka
nikatizama nyuma yangu sikuona mtu,
nikachukua zile Pesa harakaharaka, ATM
na ile pochi.
Ile natoka nje kuna dada mmoja alikuwa
anakuja kwa kasi maeneo yale nikapata
uoga nikamuuliza "Samahani dada, kuna
kitu umesahau humu", yule dada
hakunijibu kitu kaingia kwenye chumba
cha ATM akachomeka Kadi kutoa hela
mi nikaondoka zangu fasta kuelekea
home.
Nimefika home nikajifungia ndani na
kuzibwaga zile pesa kitandani,
nikafungua wallet nikakuta imejaa
dollar, Vipodozi, iphone na ki-Nokia
kidogo cha tochi, ATM Card mbili za
Benki tofauti ambazo zilikuwa
zimezungushiwa karatasi iliyokuwa na
namba za siri za ATM zote, moyo
ukanilipuka paaaa!!! Nikaona bora
Nipumzike kwanza kitandani!!
Muda si mrefu ile iphone ikaanza kuita,
nilipoangalia halikutokea jina nikaona
bora nipokee nimsikilize anasemaje,
ilikuwa sauti ya kike iliyoongea kwa
huzuni kwa kubembeleza huku akilia na
alijitambulisha vizuri kuwa ile mali ni ya
kwake! Huruma ilinijia nikamwelekeza
nilipo aje kuchukua...
Hakuchukua muda akawa amefika nami
nikamkabidhi vitu vyote naye
akavihakiki na kukuta viko sana: Milioni
3 za Kibongo na Dollar 500. Dada
kanishukuru na kunipa ile Millioni 3 ya
kibongo mi nikazikataa kwasababu ni
mali yake na alizisahau tu.
Alinitoa hofu kwa kunisihi nichukue tu,
mi kama binadamu mwenyezi Mungu
atanilipa, nikakataa... Mwishowe
akaomba namba yangu na kuondoka
zake, akawa ameniacha ndani huku njaa
sasa nikaanza kuisikia, nilikuwa na buku
mbili nikaenda kula viepe kavu na soda
nikawa powa.
Sasa jana kanipigia simu kuwa anakuja
nimsubiri, dakika tano tu akanipigia tena
kuwa ameshafika yupo nje yupo ndani
ya Prado mpyaa nikaingia tukaondoka
akaenda kunionyesha kwake kisha
tukaelekea kwenye nyumba nyingine
iliyokuwa ndo imekamilika kujengwa
akaniambia hii itakuwa yako
akanikabidhi baadhi ya nyaraka na
funguo zote sikuamini...!!
Akanisindikiza kwangu, kufika home
ananiambia hiyo gari (Prado) nayo
ananiachia ni kwa mema tu
niliyomfanyia, ndani ya ile gari kulikuwa
na brifcase iliyokuwa na pesa
akaniambia pia hii pesa itakuwa yako ya
kuanzia maisha, na kumbe yule dada
alikuwa kanipenda akanikumbatia kwa
nguvu nikiwa pale kwenye seat oooh!!
umasikini baibai...
Akiwa kanikumbatia akihema kwa kasi
juu ya kifua changu. Mara nikahisi kubanwa na haja ndogo, nikakimbia fasta chooni na kuanza kukojoa, nasikia raaaha mkojo hauishi mara nikahisi mtu
akinishika begani na  kuniita kwa sauti.
"Anko ankoo we ankoo... amka unakojoa kitandaniii!!!".
"ALIKUWA MTOTO WA SISTA ALIKUWA
ANANIAMSHA !!"
Kumbe ndotooo mweeeh

Monday, April 4, 2016

Hali ya hewa

BOY: hellow baby

GIRL: Yes hubby

BOY: Unaona hali ya hewa kimvua kinashawishi...

GIRL: haswaaa tena kwa kilimo cha maharage....

Wednesday, March 30, 2016

Maisha yamenishinda

Jamaa kamkuta mwanamke mmoja pale Ferry analia,

JAMAA: Nini shida mama angu?

MDADA:Heri nife, maisha yamenishinda

MJAMAA: Huna haja ya kufa, sikiliza mimi ni baharia na meli yetu inaenda Ulaya leo, kama unataka ingia kwenye boksi nikakufiche stoo, meli ikitia nanga Ugiriki, nakutoa ukatafute maisha huko. Bibie akaona heri hilo akaingia kwenye boksi, jamaa akambeba na mdada akajikuta yuko kwenye stoo moja wapo katika meli, jamaa akawa anamletea chakula kila siku na mara nyingine yeye mwenyewe analala huko kwenye hako kastoo kama binadamu wengine walio kamilika walikuwa wanafanya na ya kwao huko huko kwahyo safari ilikuwa nzuri hasa kwa jamaa, kila mara akimhakikishia mdada kuwa wameshapita visiwa vya Komoro, siku nyingine akimwambia wako India. Zilipita wiki mbili ndipo yule mdada akagundulika na nahodha wa chombo hicho.

NAHODHA:We unafanya nini humu?

MDADA:Chonde naomba msinitupe baharini, nilindeni mkifika Ugiriki mnishushe

NAHODHA: Unajua mbona sikuelewi? Mdada akalazimika kumueleza nahodha ishu nzima.

NAHODHA:Dah wala usipate taabu sikutupi popote, ila jamaa yako kakudanganya hii si meli ya kwenda Ulaya ni pantoni ya kwenda Kigamboni, umekuwa unazunguka hapa hapa Dar siku zote hizo, haya tukifika Kigamboni  shuka...

My relationship

Kuna wakati WADADA naona hawako seriously.... Unakuta mtu anaomba Mungu daily mpaka kwenye status anaandika "GOD BLESS MY RELATIONSHIP "........wakat huo ana date na wanaume 11......🏻sasa si bora aseme God bless my TEAM

Kifo sio kizuri

Hizi mila zingine sio nzuri.......

Juzi nimeenda kuzika rafiki yangu huko kijijini kwao, sasa utaratibu ni kua baada ya kuzika mzee wa kimila hua anaamka na kutangaza atakayefata kufa mkiwa bado eneo la kaburi. Mzee huyo alipoamka akasema mtu wa kwanza kutoka eneo la kaburi ndio atakaefata kufa. Leo siku ya tatu bado tunazunguka zunguka tu hapa kaburini pamoja na yule mzee...kweli kifo sio kizuri...

Mwalimu

Mzee: Dereva ongeza sauti tumsikilize Mwalimu Nyerere!!

Dereva: ungemsikiliza mwalimu wako miaka iyo saivi ungekua na gari yako.

Sunday, March 20, 2016

Frank amefariki

Mume katoka mihangaikoni na kurudi nyumbani anamkuta Mke wake ana huzuni na majonzi huku macho yake Yakiwa yamevimba kwa kulia.

mume: Mbona una hali hiyo mamaa!?
Mke: Frank amefariki.

Kwa hali aliyomkuta nayo ikabidi amuache apumzike aakatoka zake na kwenda varandani kupata chakula.

Mume akaamua kumuuliza dada wa nyumbani.... na kujibiwa hajala amejifungia chumbani tokea aliporudi kazini...

Mume akabaki na mawazo tele juu ya Frank aliyefariki ni nani!!???? Akiangalia anamarafiki na ndugu wanaoitwa Frank. Akapiga moyo konde nakuingia kulala.

Asubuhi wakiwa mezani wanakunywa chai.

Mume: huo msiba ni wa Frank gani na unafanyikia wapi ili nipange ratiba zangu za leo.

Mke: Frank Xavier

Mume: ndio nani huyo mbona hilo jina sijawahi kulisikia?

Mke: si yule wa Kwenye ISIDINGO

Mume: ..*¤*.*¤.¤..¤.*

Saturday, March 19, 2016

Kitambulisho

MJINI SHULE!!
Chiz kaokota elf kumi jamaa mmoja aliekuwa anapita zake akamuona
JAMAA; oy samahan hicho ni kitambulisho changu!
CHIZI: Ww hata kama cna akil vzur hich xo kitambulisho ni ela ww
JAMAA: angalia vzur!
CHIZI: kama kwel n kitambulish chako w unaitwa nan?
JAMAA; benki kuu ya tanzania
CHIZI: ulizaliwa mwak gan?
JAMAA: mwaka 10000
CHIZI: dah kwel chako samahan kwa usumbuf
JAMAA: aina noma ukiviona vingine basi unitafute
CHIZI:poa

Friday, March 18, 2016

Mama mkwe

Mama mkwe kamkuta mkwe (mume wa bintiye) sebuleni akiwa kafura na kapandisha hasira anadai ataua mtu.

Mama Mkwe: Mwanangu kwani kuna nini jamani?
Jamaa: Leo namuua mwanao, mshenzi sana.
Mama Mkwe: Tulia jamani, kimetokea nini?
Jamaa: Mwanao mshenzi sana, nilikuwa nimesafiri, nikamtumia meseji kuwa nakuja, eti bado leo nimefika nimemkuta na mwanaume kwenye kitanda chetu, dharau gani hii, sikubali leo tunagawana majengo ya serikali, yeye anaenda kulala Muhimbili mi naenda kulala Segerea
Mama Mkwe: Subiri kwanza, mwanangu hayuko hivyo lazima kuna maelezo fulani kuhusu hili ngoja nimuulize...mama mkwe akamfwata mwanawe na baada ya muda akarudi sebuleni.
Mama Mkwe: Unaona, nilijua mimi lazima kuna sababu. Kumbe mwenzio hakupata ile meseji uliyomtumia.

Thursday, March 17, 2016

Mkulima

Mkulima Jipu......

MWANDISHI: Wewe unawalisha ng'ombe chakula gani?,
MKULIMA: Ng'ombe yupi Mweupe au Mwekundu?
MWANDISHI: Ng'ombe mweupe
MKULIMA: Ninamlisha nyasi na viguta vya mahindi,
MWANDISHI: Na mwekundu??
MKULIMA: vilevile nyasi na viguta vya mahindi,
MWANDISHI: ahaa sawa,na sehemu ya kulala ni wapi?
MKULIMA: Ng'ombe yupi mweupe au mwekundu?
MWANDISHI: Mweupeee!!!
MKULIMA: Mweupe ninamlaza bomani kulee,
MWANDISHI: na mwekundu?
MKULIMA: vilevile ninamlaza na mwenziwe!!!!
MWANDISHI: Hii sehemu yote majumba mengi, wakienda kulisha unafanyaje?
MKULIMA: Yupi mweupe au mwekundu?
MWANDISHI: Woteee!!!! {kwa hasira}
MKULIMA: Mweupe nina mfunga kamba na kumzungusha malishoni na kumrudisha,
MWANDISHI: na mwekundu vilevile?
MKULIMA: Mwekundu?, mwekundu ninamfunga
kamba na kuzunguka nae kama mwenziwe!!!
MWANDISHI: Kwanini kila mara nikikuuliza huduma za ng'ombe zako unaniuliza mweupe
au mwekundu halafu inatokea kuwa kazi zao wote ni sawa??,
MKULIMA: Kwasababu Ng'ombe mweupe ni wangu,
MWANDISHI: Na mwekundu?
MKULIMA: Ni wangu vilevile!!!!!

Wednesday, March 16, 2016

Kazi

WAKUU WA MIKOA wamepewa siku 15 tu wahakikishe hakuna vijana watakao kaa bila kazi.

Kama kijana huna kazi unawekwa ndani.. ukitoka unajikuta huna kazi unarudishwa tena ndani..

Ukitoka unakuta masharti ya kazi uwe hujawahi kufungwa jela. . Unakosa hio kazi alafu unarudishwa tena ndani.🤓🤓

Tuesday, March 15, 2016

Book-keeping

Katika pitapita za JAMBAZI ucku
Alisikia watu wakibishana
kuhusu MILIONI 50,
mmoja
anasema ziweke kwa Nathan
Mwingine akasema tuweke
Bank.
Jambaz kusikia hivyo akaamua kuvunja
mlango,
Ile
kuingia akakuta wanafunzi
wana solve Book-keeping..