tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Thursday, January 29, 2015

ATM

Bishoo aliingia kwenye chumba cha mazoezi ya viungo, akamuuliza mwalimu: ‘nataka kuvutia wasichana, natumia mashine gani?

Mwalimu wa mazoezi: tumia ATM

Msichana wa Kitanzania.

Msichana wa kizungu ataandika facebook: “nakupenda sana Tom”…. Msichana wa kitanzania nae ataandika: “nakupenda sana ……….. unajijua  mwenyewe sio lazima nikutaje”. Lini wasichana wa kitanzania wataacha kuuwa ndege wengi kwa jiwe moja?

kitu gani unataka.

Unamuuliza msichana wako kitu gani anataka, anakujibu pesa unakasirika. Ni suala la ufahamu na uelewa tu.

hajui kupika

Kama hujawahi kudokoa nyama kwenye sufuria mama yako akiwa anapika basi tambua hajui kupika.

girlfriend

If you have $20 and your girlfriend has $20,

that just means your girlfriend has $40

Mshauri wa Mahusiano.

Dear Aunt,
Naomba msaada wako nifanye nini? Mimi ni mke
wa mtu, na mume wangu tunapendana sana. Juzi
niliondoka kwenda kazini nikamuacha mume
wangu ana angalia TV. Sikufika mbali gari ghafla
likazima, nikalazimika kutembea kwa miguu
kurudi nyumbani nikamwambie mume wangu
anisaidie. Nilipofika nyumbani sikuamini macho
yangu baada kumkuta mume wangu na binti wa
jirani yetu. Nilimkabiri mume wangu na kwa
bahati nzuri kakubali makosa kuwa uhusiano wao
una mwaka sasa, lakini cha ajabu amesema
atalazimika kumuacha huyo binti pole pole ili
asimchanganye kisaikolojia kwa kuwa bado
mdogo. Je hii ni sawa? Nifanye nini? Naomba
ushauri wako Tafadhali.

Fransiska wa Mwenge.


JIBU
Binti yangu Fransiska,
Nimesoma kwa makini ujumbe wako, kitu
ambacho nimekiona mara moja ni hili tatizo la
gari kuzimika ghafla. Kwanini uendeshe gari na
baada ya muda mfupi lizime? Hapa kuna
matatizo kadha wa kadha ambayo yanaweza
kuwa chanzo. Inawezekana plag mbovu au uchafu
umeingia kwenye mrija unaopeleka mafuta
kwenye injin. Au pengine ni tatizo la umeme, au
fuel pump, ulicheki kama petroli ipo? Ikiwezekana
waone mafundi warekebishe hivyo nilivyovitaja.
Nategemea ushauri huo utakusaidia mwanangu.

Monday, January 26, 2015

Bado Mtama

1. Bibi kapigwa mtama na kibaka na kuporwa simu yake.

2. Bibi akaanza kumfukuza.

3. Baada ya kuona bibi hachoki kibaka akatupa simu chini na kuendelea kukimbia.

4. Bibi akaokota simu yake na kuendelea kumfukuza tena.

5. Kibaka akauliza. '' Bibi unataka nini, Simu yako c nishakurudishia?''

6. Bibi akajibu '' Bado mtama''
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

Wednesday, January 21, 2015

KUSANYA NGUO

Mume na mke wagombana, mume akamwambia mkewe KUSANYA NGUO ZAKO..... mara simu ya mke ikaita akaweka loud speaker ni babake akasema BINTI YANGU ILE BEACH PLOT ISHAUZIKA, KESHO NTAWAPA MILIONI SITINI MFUNGUE MRADI NA MUMEO... ikakatika, mke akaanza umenambia nikusanye nguo kisha iweje? KUSANYA NGUO ZAKO UNIPE NIKUFULIE MKE WANGU....

Nasajili line

Vuta picha umelala mida Ya alfajiri hivi... Usingizi ule wa kukesha jana yake, halafu kuna mtu anakuja kukugongea mlango kwa fujo sana kwenye mida ya kama saa moja moja hivi. Ile unaamka na hasira zako kwenda kumfungulia unajikwaa kidole cha mwisho cha mguu ktk kona ya kitanda ile ndiiii.. kugeuka unaparamia ndoo za maji yanamwagika. mara unateleza ktk yale maji unaangukia meza unaangusha tv, deki na ww chini mara waya wa umeme unakupiga short mgongoni unafika mlangoni na maumivu ya kidole na uchovu + hasira+hasara na short juu unakutana na jamaa anakwambia nasajili line za tigo & Vodacom!
UTAFANYAJE!?

Tuesday, November 11, 2014

Golden Words By A Wise Man

1. "If you want to change the world, do it when you are a bachelor. After marriage, you can't even change a TV channel"

2. "Listening to wife is like reading the terms and conditions of website. You understand Nothing, still you agreed..."

3. "Chess is the only game in the world, which reflects the status of the husband. The poor King can take only one step at a time...While the mighty Queen can do whatever she likes."

4. "All men are brave. Horror movies don't scare them...But 5 missed calls from wife...surely..."

Saturday, October 25, 2014

Wahehe

TANGAZO KWA WAHEHE WOTE:
Chuo kipya kabisa cha Kihehe kimefunguliwa Kihesa, Iringa.
(HEHE SKILLS AND TECHINICAL COLLEGE OF LIFE)

Kinatangaza kozi za mwaka 2015/2016 kama ifuatavyo,
1. Kugema ulanzi miezi 6
2. Kusokota kamba za kujinyonga miezi 9;
3. Kuchagua mbwa anaefaa kuliwa na mapishi yake miezi 8;
4. Kuongeza hasira miezi 10-12Atakae.
 jiunga mapema atapewa kozi ya upishi wa Mkunungu pamoja na uoshaji wa Mbeta.

Wasambaa

Wasambaa wanapenda sana kazi zao hasa udeeva (udereva). Ukimkuta msambaa msukuma mkokoteni muulize kazi yake utasikia mimi deeva.

Wazaramo

siri ya wazaramo kutopenda shule ni kutokana na wao kuzaliwa Da es salaamm hivyo hawaoni sababu ni kwa nini waende shule, bali wa kwenda shule ni watu wa mikoani sababu wao wanasoma ili waje Dar es Salaam.

utasikia wanasema

wazaramo: wewe unasoma uje darichalama, mie nisome niende wapi?


(wakati ule karibu kila kitu kilikuwa Dar, ajira Dar, Chuo Kikuu Dar, nk.)

Mfupi

Rafiki yake Jost ni mfupi mpaka akikaa kwenye kiti badala ya kukunja nne, yeye anakunja mbili

Wednesday, September 24, 2014

M-pesa na tigo pesa

Jost: Dada Mambo?
Chaupele: Powa.
Jost: Samahani, nimevutia na wewe nataka tuwe marafiki, Hivi Uko Facebook?
Chaupele: Hapana.
Jost: Twitter?
Chaupele: Sipo.
Jost: Whatsap?
Chaupele: Sipo.
Jost: Instagram?
Chaupele: Sipo.
Jost: Eeeeh Sasa upo kwenye mtandao gani sasa?
Chaupele: Niko M-pesa na tigo pesa.