tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Thursday, January 29, 2015

Mshauri wa Mahusiano.

Dear Aunt,
Naomba msaada wako nifanye nini? Mimi ni mke
wa mtu, na mume wangu tunapendana sana. Juzi
niliondoka kwenda kazini nikamuacha mume
wangu ana angalia TV. Sikufika mbali gari ghafla
likazima, nikalazimika kutembea kwa miguu
kurudi nyumbani nikamwambie mume wangu
anisaidie. Nilipofika nyumbani sikuamini macho
yangu baada kumkuta mume wangu na binti wa
jirani yetu. Nilimkabiri mume wangu na kwa
bahati nzuri kakubali makosa kuwa uhusiano wao
una mwaka sasa, lakini cha ajabu amesema
atalazimika kumuacha huyo binti pole pole ili
asimchanganye kisaikolojia kwa kuwa bado
mdogo. Je hii ni sawa? Nifanye nini? Naomba
ushauri wako Tafadhali.

Fransiska wa Mwenge.


JIBU
Binti yangu Fransiska,
Nimesoma kwa makini ujumbe wako, kitu
ambacho nimekiona mara moja ni hili tatizo la
gari kuzimika ghafla. Kwanini uendeshe gari na
baada ya muda mfupi lizime? Hapa kuna
matatizo kadha wa kadha ambayo yanaweza
kuwa chanzo. Inawezekana plag mbovu au uchafu
umeingia kwenye mrija unaopeleka mafuta
kwenye injin. Au pengine ni tatizo la umeme, au
fuel pump, ulicheki kama petroli ipo? Ikiwezekana
waone mafundi warekebishe hivyo nilivyovitaja.
Nategemea ushauri huo utakusaidia mwanangu.