tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Tuesday, January 12, 2016

Zimwi

RIWAYA YA MAANDISHI:

Mheshimiwa mmoja baada ya kupata cheo akapewa nyumba mitaa ya watu wenye pesa. Akahamia huko akiwa na mke na mwanae. Siku moja mwanae aliyekuwa kazoea maisha ya Uswazi akawa anawinda ndege na manati kwenye uwanja wa jumba lao, bahati mbaya jiwe likapitiliza na kwenda kuvunja kioo cha nyumba ya jirani.

Mheshimiwa na mkewe wakaamua kumfuata mwenye nyumba wakamuombe msamaha. Walipogonga mlango akafungua mbaba mmoja akawakaribisha kwa heshima, wakaingia na kuanza kujieleza. 'Samahani sisi tumehamia karibuni hapo nyumba ya pili, mwanetu kavunja kioo chako kwa bahati mbaya, tumekuja kuomba msamaha na kuona kama tunaweza kutengeneza'.

Mwenyeji wao akawaomba wakae kisha akawaambia, 'Naomba niwahadithie kitu. Kwanza mimi nawashukuru nyinyi na mtoto wenu. Mwenye nyumba hii ni mchawi mkubwa sana, mimi ni ZIMWI alikuwa amenifungia kwa zaidi ya miaka 20 kwenye kichupa ambacho kilikuwa kwenye dirisha lililovunjwa. Baada ya dirisha kuvunjika na chupa nacho kikavunjika nami nimekuwa huru. Kwa hiyo kwa shukurani ombeni chochote mtakacho nitawapa, nina uwezo huo'

Hapo hapo muheshimiwa akauliza tena,'Yaani kitu chochote?' Akajibiwa 'Ndio'. Basi pale pale akasema, ' Mimi naomba bosi wangu asinifuatilie na madhambi yangu ofisini yasahaulike kabisa na pia niwe bilionea mpaka nife' Akajibiwa ,' Hilo jambo dogo sana kwangu, hakufuati tena na kesho utaamka tajiri. Mama nae akaomba vyake, 'Mi nataka niwe na nyumba kila nchi duniani na niwe na biashara Dubai na China na Hong Kong' Akajibiwa, 'Umepata mama, kuanzia kesho hayo ni yako.

ZIMWI likasema "Mimi nawashukuru kwa uhuru wangu lakini nina kaombi kadogo".  Mheshimiwa haraka akajibu, 'Sema tu wewe ni kama ndugu yetu sasa' Basi ZIMWI likasema, 'Naomba mkeo abaki hapa kama masaa mawili tu, unajua kifungo nilichofungwa kilinizuia kila kitu, hata mke sijapata kipindi chote hicho. Nikimaliza tu hilo nitaondoka kurudi kwetu Uzimwini hamtaniona tena, itakuwa siri yetu'.

Mme na mke wakajadiliana wakaona utajiri waliopata ni mkubwa sana, na hilo jambo ni dogo sana la mara moja tu tena kwa siri, wakakubali sharti. Mke akabaki pale kwa masaa kadhaa. Shughuli ilipokwisha, mama wa watu akiwa anajitayarisha kurudi kwa mumewe kichwani akiwaza utajiri, ZIMWI likakohoa kidogo na kumuuliza yule mama, 'Samahani una miaka mingapi na mumeo ana miaka mingapi?" Mama wa watu akajibu, 'Mie nina miaka 40 mume wangu ana miaka 46' Yule mbaba Zimwi akacheka sanaa, na kusema "Sasa nyinyi wakubwa wazima mpaka leo mnaamini stori za  MAZIMWI?