Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baba, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani ?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa. Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na Manyani baadae tukawa Binadamu. (Mtoto akarudi kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa Manyani mwanzo? Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao.
tangazo one
Abidal
karibuni
ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.