tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Friday, January 29, 2016

Madevu

Jamaa akiwa nyumba ndogo karelax na Mdada, Mdada kwa sauti laini akaanza;
MDADA: Jamani lini utanyoa hizo ndevu, mi sizipendi
SOUD: Bwana ziache mke wangu anazipenda sana hatutaelewana nikizinyoa!
MDADA: Nyoa jamani, au hunipendi?
SOUD: Nakupenda, lakini kwa nini huzipendi?
MDADA: Unajua we handsome boy sana mpenzi, mi nataka niwe nauona uso wako wote swiry…
Soud hatimae akanyoa ndevu zote. Baadae akarudi nyumbani usiku akinyata taratibu na kufanikiwa kupanda kitandani wakati anaanza kulala tu. Mke wake akiwa usingizini akageuka na kumgusa mashavu,
MKE: We JULIUS, huogopi kufa, mume wangu atarudi muda wowote, ondoka haraka bwana!sije ukanivunjia ndoa yangu.....

Friday, January 22, 2016

Nimewaza tu

Nimekaaa nikawaza tu embu ngoja nisaidieni jamani..

Kama uko kwenye mapenzi na mtu zaidi ya mmoja na unasema wote unawapenda basi huo sio moyo tena ni memory card...

Japo kuna watu wana hard disk kabisa

Kuoa ni majaliwa

Kuna vitu ukiona kijana wakiume anavifanya Gheto ujue kuoa ni majaliwa
1.anapika chapati za kusukuma Gheto
2.Anakuna nazi Gheto
3.Anapika makande gheto
4.Ameweka midori kitandani
5.Ameweka kadi mezani
6.Ananunua gunia la mkaa anaweka gheto....
7. kaweka dressing table
8. kanunua vyombo vya ndani vya kutosha.
9. ananunua viungo vingi sana sokoni
10. anapenda kulakula hovyo

Hayo ni mambo yanayo bainisha kuwa upatikanaji wa mke kwa upande wake ni mdogo

Tuesday, January 19, 2016

Magonjwa

Teacher :: Tuandike aina ya magonjwa mbali mbali
Paul::H.I.V
Eliud: cholera
Chrispin: malaria...
Deborah: typhoid
Edson: /

Teacher: Sasa wewe Edson ndo ugonjwa gani huo umeandika  /?
Edson: stroke

Kazi za wazazi

Mwalimu kauliza swali darasani
wanafunzi wataje
kazi za wazazi wao:
TINA: mimi baba yangu
mfanyabiashara mama
yangu mwalimu.
MWALIMU: Safi, haya juma
JUMA: Baba yangu dereva mama
yangu hafanyi
kazi.
MWALIMU: Vizuri, haya Zogo.
ZOGO: Mimi mama yangu malaya
anajiuza baba
simjui.
MWALIMU: Pumbavu wewe, nenda
ofisini kwa
mwalimu mkuu ukamueleze upuuzi
wote
uliosema hapa. Zogo anaenda ofisini
anarudi
huku anatabasamu na anakula
biskuti.
MWALIMU: Mwalimu mkuu kakupa
adhabu gani?
ZOGO: Kaniambia nimpe namba ya
mama...

Saturday, January 16, 2016

Kuoa ni majaliwa

Kuna vitu ukiona kijana wakiume anavifanya Gheto ujue kuoa ni majaliwa
1.anapika chapati za kusukuma Gheto
2.Anakuna nazi Gheto
3.Anapika makande gheto
4.Ameweka midori kitandani
5.Ameweka kadi mezani
6.Ananunua gunia la mkaa anaweka gheto....
7. kaweka dressing table
8. kanunua vyombo vya ndani vya kutosha.
9. ananunua viungo vingi sana sokoni
10. anapenda kulakula hovyo

Hayo ni mambo yanayo bainisha kuwa upatikanaji wa mke kwa upande wake ni mdogo

Friday, January 15, 2016

Nyumba inauzwa

Kuna nyumba inauzwa  milioni mbili ipo ndani ya fensi ya matofali inaeneo lenye 40m x 35m inavyumba nane, na sehemu ya kupaki gari, ina maji na umeme.  Ipo mita 100 kutoka barabarani ina x lakini inafutika.

Tuesday, January 12, 2016

Zimwi

RIWAYA YA MAANDISHI:

Mheshimiwa mmoja baada ya kupata cheo akapewa nyumba mitaa ya watu wenye pesa. Akahamia huko akiwa na mke na mwanae. Siku moja mwanae aliyekuwa kazoea maisha ya Uswazi akawa anawinda ndege na manati kwenye uwanja wa jumba lao, bahati mbaya jiwe likapitiliza na kwenda kuvunja kioo cha nyumba ya jirani.

Mheshimiwa na mkewe wakaamua kumfuata mwenye nyumba wakamuombe msamaha. Walipogonga mlango akafungua mbaba mmoja akawakaribisha kwa heshima, wakaingia na kuanza kujieleza. 'Samahani sisi tumehamia karibuni hapo nyumba ya pili, mwanetu kavunja kioo chako kwa bahati mbaya, tumekuja kuomba msamaha na kuona kama tunaweza kutengeneza'.

Mwenyeji wao akawaomba wakae kisha akawaambia, 'Naomba niwahadithie kitu. Kwanza mimi nawashukuru nyinyi na mtoto wenu. Mwenye nyumba hii ni mchawi mkubwa sana, mimi ni ZIMWI alikuwa amenifungia kwa zaidi ya miaka 20 kwenye kichupa ambacho kilikuwa kwenye dirisha lililovunjwa. Baada ya dirisha kuvunjika na chupa nacho kikavunjika nami nimekuwa huru. Kwa hiyo kwa shukurani ombeni chochote mtakacho nitawapa, nina uwezo huo'

Hapo hapo muheshimiwa akauliza tena,'Yaani kitu chochote?' Akajibiwa 'Ndio'. Basi pale pale akasema, ' Mimi naomba bosi wangu asinifuatilie na madhambi yangu ofisini yasahaulike kabisa na pia niwe bilionea mpaka nife' Akajibiwa ,' Hilo jambo dogo sana kwangu, hakufuati tena na kesho utaamka tajiri. Mama nae akaomba vyake, 'Mi nataka niwe na nyumba kila nchi duniani na niwe na biashara Dubai na China na Hong Kong' Akajibiwa, 'Umepata mama, kuanzia kesho hayo ni yako.

ZIMWI likasema "Mimi nawashukuru kwa uhuru wangu lakini nina kaombi kadogo".  Mheshimiwa haraka akajibu, 'Sema tu wewe ni kama ndugu yetu sasa' Basi ZIMWI likasema, 'Naomba mkeo abaki hapa kama masaa mawili tu, unajua kifungo nilichofungwa kilinizuia kila kitu, hata mke sijapata kipindi chote hicho. Nikimaliza tu hilo nitaondoka kurudi kwetu Uzimwini hamtaniona tena, itakuwa siri yetu'.

Mme na mke wakajadiliana wakaona utajiri waliopata ni mkubwa sana, na hilo jambo ni dogo sana la mara moja tu tena kwa siri, wakakubali sharti. Mke akabaki pale kwa masaa kadhaa. Shughuli ilipokwisha, mama wa watu akiwa anajitayarisha kurudi kwa mumewe kichwani akiwaza utajiri, ZIMWI likakohoa kidogo na kumuuliza yule mama, 'Samahani una miaka mingapi na mumeo ana miaka mingapi?" Mama wa watu akajibu, 'Mie nina miaka 40 mume wangu ana miaka 46' Yule mbaba Zimwi akacheka sanaa, na kusema "Sasa nyinyi wakubwa wazima mpaka leo mnaamini stori za  MAZIMWI?

Ukoo wao

Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baba, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani ?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa. Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na Manyani baadae tukawa Binadamu. (Mtoto akarudi kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa Manyani mwanzo? Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao.

Familia za watu

Ati john is 10 years older than his father, his mother is 40 years old.,20 years younger than john.,find the Age of
1.john
2.father
3.mother

Hii swali nilikuwa naruka..Sio ati ujinga...ni vile tu sipendi kuingilia mambo ya familia za watu..

Kande na Parachichi

Unaenda hotelini unaona menu imeandikwa:
Sauteed white corn, rare lucy beans, garnished with rift potatoes & topped with organic unprocessed guacamole.

Price: TSH 44,000

Unaagiza! Ukiletewa ndio unagundua kwamba: Ni Kande  na parachichi.....

Monday, January 11, 2016

Inside the bank

Jost goes on the ATM and withdraw all the money from the ATM.

Then he goes inside the same bank and deposit all the money he withdrew from the ATM, telling the Teller, "my money is not safe outside in the ATM. People are just withdrawing anyhow and they might end up withdrawing what is mine. Keep my money inside the bank please."

Monday, January 4, 2016

English lesson

During an English lesson, the teacher instructed his students to write a composition.

QN: Assume you are in a war, write a story?

One student did not write any thing & kept seated. The Teacher got puzzled, walked to the student's desk & asked him why he was not doing the exercise.

The student replied,  "I was killed immediately at the beginning of the war".