tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Wednesday, September 19, 2012

Mtanzania na mkenya

Mtanzania na mkenya waliingia supermarket moja jijini DSM.Walipotoka nje,mkenya akawa anajigamba kwamba wakenya ni wajanja kuliko wa-TZ huku akimuonesha m-TZ chocolate tatu alizokwiba supermarket.M-bongo akamshawishi mkenya warudi tena ndani ya supermarket ili naye akamuoneshe ustadi wake.Walipofika tu ndani,m-TZ akamwambia mhudumu,'nataka kukuonesha mazingaombwe,hebu niletee chocolate tatu!'.Yule mhudumu akamletea chocolate tatu,jamaa akazila zote mbele ya mhudumu halafu akasema,'unaona mhudumu,mwenyewe umeshuhudia nimekula chocolate tatu lakini amini usiamini,chocolate zako ziko mfukoni kwa huyu jamaa'.Mhudumu akamkagua mkenya mfukoni then akachukua chocolate zake zote tatu.