tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Saturday, October 25, 2014

Wasambaa

Wasambaa wanapenda sana kazi zao hasa udeeva (udereva). Ukimkuta msambaa msukuma mkokoteni muulize kazi yake utasikia mimi deeva.

Wazaramo

siri ya wazaramo kutopenda shule ni kutokana na wao kuzaliwa Da es salaamm hivyo hawaoni sababu ni kwa nini waende shule, bali wa kwenda shule ni watu wa mikoani sababu wao wanasoma ili waje Dar es Salaam.

utasikia wanasema

wazaramo: wewe unasoma uje darichalama, mie nisome niende wapi?


(wakati ule karibu kila kitu kilikuwa Dar, ajira Dar, Chuo Kikuu Dar, nk.)

Mfupi

Rafiki yake Jost ni mfupi mpaka akikaa kwenye kiti badala ya kukunja nne, yeye anakunja mbili

Wednesday, September 24, 2014

M-pesa na tigo pesa

Jost: Dada Mambo?
Chaupele: Powa.
Jost: Samahani, nimevutia na wewe nataka tuwe marafiki, Hivi Uko Facebook?
Chaupele: Hapana.
Jost: Twitter?
Chaupele: Sipo.
Jost: Whatsap?
Chaupele: Sipo.
Jost: Instagram?
Chaupele: Sipo.
Jost: Eeeeh Sasa upo kwenye mtandao gani sasa?
Chaupele: Niko M-pesa na tigo pesa.

Wednesday, September 17, 2014

huna uwezo wa kupata mimba

Binti mmoja aliamua kwenda kwa dakitari baada ya kuona hapati mimba, alipofika na baada ya vipimo.
Dakitari: binti inaonyesha wewe ni mgumba kwa hiyo huna uwezo wa kupata mimba.
Binti: jamaniii (huku akianza kutokwa na machozi).
Dakitari: usilie ngoja tujaribu kuangalia chanzo cha tatizo ni nini tuone kama kuna msaada.
Binti: naomba unisaidie.
Dakitari: usijali, lakini hili tatizo linaweza kuwa la kurithi, kwani mama yako aliwahi kuzaa?
Binti: sijui labda nikamuulize.
Dakitari: …………….

Binti:……………

Chaupele

Jost: mambo mrembo, mbona kimya?
Chaupele: unanitaka unagari lakini?
Jost: gari?
Chaupele: ndio gari.
Jost: sina gari.
Chaupele: basi acha kunifuata fuata hunifai
Jost: vipi kwani we unalo?
Chaupele: sina gari.
Jost: una sehemu ya kuosha magari au garage?
Chaupele: sina
Jost: baba yako analo gari?
Chaupele: Hana gari.
Jost: sasa wewe mazoea ya kupanda gari umeyatoa wapi?

Chaupele: nyooooo….. mbwa weee unikome!

baba ni mbahili sana

Baba alikuwa na tabia ya kulala na dada wa kazi, siku moja mtoto wake wa kiume akamfumania:
Baba: Mwanangu, ebu chukua hii Shs 500 halafu usimuambie mama yako kuwa nimelala na dada.

Mtoto: sitaki, we baba ni mbahili sana, mbona mama akilala na mlinzi ananipaga Shs. 1,000?

Monday, July 14, 2014

mara ya mwisho kuongea na boyfriend wako lini?

binti mmoja wa kidato cha kwanza akiwa anatoka shule simu yake iliita alipoitoa akaona ni namba ngeni kwake. alipopokea akakutana na sauti ya kiume na ikamuuliza
mwanaume: Mara ya mwisho kuonana na boyfriend wako ilikuwa lini?
bint: jana jioni nikiwa natoka shule.
mwanaume: kumbe we mtoto una wanaume ngoja urudi nyumbani utanitambua, maana mama yako alikuwa ananiambia nambishia.
bint: baba nilikuwa natania tu, nilijua ni wavulana wanaonisumbua ndio maana nikasema hivyo.
baba yake akakata simu, yule binti akiwa anakaribia kufika nyumbani simu ikaita tena na ninamba mpya na tofauti na ya mwanzo, alipopokea akasikia tena sauti ya kiume.
mwanaume: una boyfriend?
binti: hapana sina
mwanaume: kumbe hunipendi eeh yaani unanikana?
binti: samahani mpenzi nilijua baba yangu, nakupenda sana na ndio maana nikatoroka jana jioni na kuja kwako.
mwanaume: pumbavu, utanikoma nilitaka kupata ushahidi zaidi, juu ya huo upumbavu wako.
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

kanyonyeshe mtoto

MKE: Mbona hawa Brazil hawamchezeshi Neymar ?
MME: Aliumia mechi iliyopita, hawezi kucheza
MKE: Mbona hawajamkodiMESSI??
MME: Hairuhusiwi kukodi... izo sio nyumba za kupanga
kwamba unahamia tu,mpaka uwe una uraia waNchi
yako.
MKE: Mbona hadi wanawake wanacheza umo
uwanjani?
MME :Wapo wapi hao wanawake?
MKE: Si hao wa Brazil wenye
nywele ndefu?
MME: hapana hao ni Wanaume wanaitwa David Luiz na
WILLIUM
MKE: Mbona hao wengine wanapiga Penati 5
wenyewe? eti Refa anapendelea?
MME: Hakuna Penati hapo ni magoli,Brazil wamezidiwa
wanafungwa.
MKE: Mbona Goli 7 ni nyingi na ni Dk ya 80, kwanini
refa
hamalizii tu hapo si bingwa alishajulikana.
MME: Sheria ya mpira mpaka Dk 90 zitimie..
MKE: Huu si mpira wa miguu??
MME: Ndio we unaonaje?
MKE: mbona huyo mwingine anadaka na mikono?
MME: huyo ni kipa
MKE: kwanini huyu Kipa wa Brazil asikimbie na mpira
hadi goli
jingine alafu afunge apunguze magoli au hajui huo
ujanja?
MME: kanyonyeshe mtoto ameamka...
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

Wednesday, July 9, 2014

Unaumwa nini

Kuna babu mmoja alikutwa stendi ya mabasi analia sana. Wasamaria wema wakaamua kumsaidia yule babu lakini kila walipokuwa wakimwuliza, “Babu unalilia nini?” akawa hasemi anaendelea kulia tu, wasamaria wema wakaamua kumbeba hadi hospitali. Walipofika hospitali daktari akamwuliza babu tatizo lake ili aweze kumsaidia,
Daktari: Mzee unaumwa nini?
Babu: (Akaendelea kulia kwa muda)
Daktari: Eti babu yangu nini kinakusumbua? Unaumwa nini nikutibu?

Babu: SIUMWI ILA VIATU VINANIBANA!!!

wamekubaliana na baba

Baba, mtoto wake na jiran yao,walikuwa wawindaji wa wanyawa pori, kwa kutumia mtego mkubwa wa nyavu (IKILA). Kawaida ya mtego huo mmoja akae mwishoni mwa urefu na mwingine nae mwshoni vilevlie. Sasa mzee akawa atatafuta wanyama kila kichaka, bahati nzuir akatokea mnyama aina ya NGIRI, mnyama huyu huwa ana meno mawili yaliyo tokokeza nje, akaelekezwa na mzee kwnye mtego, akalenga upande wa mtoto, badala ya kumuuwa, akamkwepa. Alpoulizwa vipi wewe? kasema, mnyama mwenyewe alikuwa anacheka, mi nikadhani yawezekana kuna maelewano wamekubaliana na baba.

Dawa ya kuacha Pombe

Mlevi nae akaenda kupata dawa ya kuacha pombe, akambiwa awe anameza vidonge viwili mara tatu kwa siku, akamuuliza dr, hizi dawa kwani zinamadhara nikimeza alafu nikanywa pombe?

dawa ya kuacha bangi

Mshikaji alienda kwa Dr kupata dawa ya kuacha bangi, dr akamwambia awe anameza mara tatu kwa siku, mshikaji akamuuliza niwe nameza baada ya kuvuta bangi au kabla?

kama Mvua inanyesha

Jamaa alikuwa Ktandani na mke wa mtu mwenyewe akarudi na kugonga Mlango Mke akamwambia Jamaa pitia dirishan Kimbia, jamaa akaanza kubisha eti nje Kuna Mvua, Mwanamke akamwambia Mme wangu ana hasira na ana Pisto, jamaa akachukua Nguo zake na kuruka dirishani na Kukimbia kufika Barabarani akakuta watu wengi wanakimbia wako kwenye Mashindano ya mbio nae akajiunga mmoja akamuulza mbona unakimbia Uchi? Jamaa akajibu napenda sana kukimbia hivi najisikia poa, mwingine akamwambia ndo ukimbie Nguo umebana kwapani? Akajbu sasa niziweke wapi? Mwingine akamuulza kwa hiyo kila ukiwa unakimbia unavaa Kondom? Jamaa huwa navaa kama Mvua inanyesha.

kufanyiwa usaili

Jost alikuwa anatafuta kazi sana... akaenda ofisi moja na kuanza kufanyiwa usaili,
Afisa: una akili timam
Jost: ndio, ninazo.
Afisa: 1 + 1 =?
Jost: 2
Afisa: nani alimuua Abraham Lincorin?
Jost: mhh! Sijui
Afisa: okey! Kalifanyie kazi hilo afu kesho urudi hapa...
Jost akaenda kwa rafik yake, akaulizwa umepata kazi?

Jost akajibu “ndio, tena nzito kweli, nashughulikia kesi ya mauaji.”