tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Wednesday, April 22, 2015

Whatsapp

Kule whatsapp kuna vituko watu na status zao;.
1. Mtu ameandika "Sleeping" , sasa leo siku
ya tano, si kishakufa huyu?
2. Mwingine kaandika "Driving" toka mwaka
jana Agosti, naona atakuwa anakaribia
Afghanistan saa hizi
3. Haya jamaa najua kalazwa anaumwa
lakini kaandika "Happy" we vipi ndugu
yangu?
4. Huyu mdada kaandika "Available". Sijui
anajua maana yake?
5. Mbosi huyu hajabadilisha status mwaka
wa pili sasa, "Hey there! I'm using
WhatsApp" sasa unadhani sijui?
Tungekutanaje kama hutumii Whatsapp?
6. Superstar wetu mmoja kaandika "Urgent
calls only". We vipi? Kwani we faya, au
ambulens au polisi?
7. Haka kabishoo kameandika "Can't talk,
WhatsApp only". Sasa una simu ya nini?
Si uitupe uwe unashinda Facebook? Simu
kazi yake ya kwanza kuongea sio
Whatsapp, pambafu we.
8. Huyu mshamba kaandika "At the movies"
wiki ya saba sasa, sinema gani ndefu
hivyo wewe? Au unafanya kazi ya kuuza
tiketi hapo sinema?
9. Dogo kaandika "At school" sasa
Whatsapp ya nini? Utapata Div O wewe
10. Mwezi wa pili sasa mchepuko umeandika
"Busy" hivi busy unafanya nini? Nikiacha
kukutumia credit utaanza kelele
11. Hahahahahaha eti "Battery about to die"
miezi sita mfululizo, badilisha hiyo betri?
Au mtaa wenu hakuna umeme miezi sita
hujachaji simu? Si kalalamikeni
TANESCO? Au nikununulie jenereta?
Unaudhi
12. Hivi najiuliza we mdada huu mwezi wa
nne sasa eti "At the gym" unajitayarisha
kwa Olympic
13. Bosi status yako ya "In a meeting"
mwezi mzima inachekesha, maliza huo
mkutano rudi kwenu.