tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Wednesday, April 1, 2015

Kibuyu

Nilipokuwa shule ya msingi, kuanzia darasa la 4
hadi la 7 maksi zangu za hesabu kwenye mitihani
zilikuwa zinacheza kwenye 03%-
08%. Matokeo yalikuwa yanatangazwa mbele ya
darasa!
Yanapotangazwa mwalimu anaanza kuwaita
wanafunzi kwa kuanzia
maksi za chini kwenda juu (0-100),
kwahiyo darasa lote linajua makaratasi yakiletwa
lazima niitwe
kama si wa kwanza basi wa pili toka chini.
Siku moja mwalimu akaanza kuita majina, mpaka
akafikia kwenye maksi 30%,40%,50%,60%,70%
bado tu mi hajaniita.
Watu wakaanza kuniangalia waliokuwa karibu
wakaanza
kuniuliza..."" Eeeh umepasua hujaitwa,
ilikuwaje??
Nlianza kuvimba kichwa, huku mwalimu
anaendelea kugawa tu makaratasi.
Yakabaki makaratasi ya watu wawili tu waliopata
80%-90% bado mi sijaitwa ...
Mara akabaki na karatasi moja mkononi...!!!!
Darasa lote macho kwangu hawaamini
kinachotokea maana bado
sijapata karatasi..
Mwishoni mwalimu akaangalia juu akashusha
pumzi, kisha
akasema... "KUNA LIKIBUYU" halijaandika jina
Limepata 0% aje kuchukua karatasi lake!!.