Siku moja punda alienda kwa SIMBA 'mfalme wa mbuga' kushitaki wenziwe
wanaomcheka na kumuita PUNDA, jina hili la punda hakulipenda kabisa
kwa sababu wenziwe wanasema jina hilo ni kwa ujinga mwingi alonao huyo
punda ndipo akaitwa punda. Mazungumzo yao yakawa hivi:
Simba: Wacha nikupe mtihani mdogo kupima akili yako kama kweli wewe ni
mjanja na mwerevu kama wenzio, ukishinda mtihani huu nitakubadili jina
na kukuita Farasi.
Punda: Nipime ujanja wangu na utanikuta ni mwerevu sana kushinda
wenzangu.
Simba: Sawa, sasa nenda mbiooooo mpaka nyumbani kwangu ukaniangalie
nipo huko au sipo nyumbani mwangu? Halafu urudi unipe jibu.
Punda: Kazi rahisi sana hiyo, nisubiri hapa nakuja sasa hivi.
Basi bwana Punda akatoka mbio hadi kwa nyumbani kwa mfalme kwenda
kumwangalia kama yupo.
Kweli Punda zuzu, sasa anakwenda kumwangalia nani wakati mfalme
mwenyewe amemuacha njiani.
Aliporudi mambo yakawa hivi:
Simba: Enhee vipi umenikuta?
Punda: Mh! Haupo.
Simba: Basi kama ndivyo, utaendelea kuitwa Punda hivyo hivyo kutokana
na akili yako ndogo. Sasa umekwenda kwangu kunitafuta vipi wakati
umeniacha hapa? Haya potea hapa haraka sana, Punda wewe! Kuanzia hapo
jina la Punda linabaki kuwa hivyo hivyo!!!