tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Monday, January 24, 2011

Shuka nikumeze

Mama mmoja alikuwa akiishi ghorofani peke yake lakini alikuwa muoga
sana . Siku moja asubuhi wakati anashuka kuelekea chini akasikia sauti
ikisema, Shuka nikumeze! Shuka nikumeze!
Mh! Yule mama kusikia vile moyo ukaanza kumwenda mbio akijua kwamba
kuna jitu kubwa ambalo ndilo linalomwambia hivyo na kwamba kweli
akishuka litammeza.
Basi akaamua kupiga simu polisi ili waje wamsaidie. Haikupita muda
polisi wakafika nyumbani kwa yule mama wakiwa wamejikoki vizuri huku
wakiwa na silaha nzito.
Cha ajabu sasa walipofika wakakutana na kichaa mmoja mdogo kadhoofika
akiwa amelala chini ya lile ghorofa, kamasi zikimtoka mithili ya dawa
ya mswaki iliyominywa huku akiimba Shuka nikumeze! Shuka nikumeze,
akimaanisha kamasi zishuke azimeze!