tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Monday, July 14, 2014

mara ya mwisho kuongea na boyfriend wako lini?

binti mmoja wa kidato cha kwanza akiwa anatoka shule simu yake iliita alipoitoa akaona ni namba ngeni kwake. alipopokea akakutana na sauti ya kiume na ikamuuliza
mwanaume: Mara ya mwisho kuonana na boyfriend wako ilikuwa lini?
bint: jana jioni nikiwa natoka shule.
mwanaume: kumbe we mtoto una wanaume ngoja urudi nyumbani utanitambua, maana mama yako alikuwa ananiambia nambishia.
bint: baba nilikuwa natania tu, nilijua ni wavulana wanaonisumbua ndio maana nikasema hivyo.
baba yake akakata simu, yule binti akiwa anakaribia kufika nyumbani simu ikaita tena na ninamba mpya na tofauti na ya mwanzo, alipopokea akasikia tena sauti ya kiume.
mwanaume: una boyfriend?
binti: hapana sina
mwanaume: kumbe hunipendi eeh yaani unanikana?
binti: samahani mpenzi nilijua baba yangu, nakupenda sana na ndio maana nikatoroka jana jioni na kuja kwako.
mwanaume: pumbavu, utanikoma nilitaka kupata ushahidi zaidi, juu ya huo upumbavu wako.
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

kanyonyeshe mtoto

MKE: Mbona hawa Brazil hawamchezeshi Neymar ?
MME: Aliumia mechi iliyopita, hawezi kucheza
MKE: Mbona hawajamkodiMESSI??
MME: Hairuhusiwi kukodi... izo sio nyumba za kupanga
kwamba unahamia tu,mpaka uwe una uraia waNchi
yako.
MKE: Mbona hadi wanawake wanacheza umo
uwanjani?
MME :Wapo wapi hao wanawake?
MKE: Si hao wa Brazil wenye
nywele ndefu?
MME: hapana hao ni Wanaume wanaitwa David Luiz na
WILLIUM
MKE: Mbona hao wengine wanapiga Penati 5
wenyewe? eti Refa anapendelea?
MME: Hakuna Penati hapo ni magoli,Brazil wamezidiwa
wanafungwa.
MKE: Mbona Goli 7 ni nyingi na ni Dk ya 80, kwanini
refa
hamalizii tu hapo si bingwa alishajulikana.
MME: Sheria ya mpira mpaka Dk 90 zitimie..
MKE: Huu si mpira wa miguu??
MME: Ndio we unaonaje?
MKE: mbona huyo mwingine anadaka na mikono?
MME: huyo ni kipa
MKE: kwanini huyu Kipa wa Brazil asikimbie na mpira
hadi goli
jingine alafu afunge apunguze magoli au hajui huo
ujanja?
MME: kanyonyeshe mtoto ameamka...
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

Wednesday, July 9, 2014

Unaumwa nini

Kuna babu mmoja alikutwa stendi ya mabasi analia sana. Wasamaria wema wakaamua kumsaidia yule babu lakini kila walipokuwa wakimwuliza, “Babu unalilia nini?” akawa hasemi anaendelea kulia tu, wasamaria wema wakaamua kumbeba hadi hospitali. Walipofika hospitali daktari akamwuliza babu tatizo lake ili aweze kumsaidia,
Daktari: Mzee unaumwa nini?
Babu: (Akaendelea kulia kwa muda)
Daktari: Eti babu yangu nini kinakusumbua? Unaumwa nini nikutibu?

Babu: SIUMWI ILA VIATU VINANIBANA!!!

wamekubaliana na baba

Baba, mtoto wake na jiran yao,walikuwa wawindaji wa wanyawa pori, kwa kutumia mtego mkubwa wa nyavu (IKILA). Kawaida ya mtego huo mmoja akae mwishoni mwa urefu na mwingine nae mwshoni vilevlie. Sasa mzee akawa atatafuta wanyama kila kichaka, bahati nzuir akatokea mnyama aina ya NGIRI, mnyama huyu huwa ana meno mawili yaliyo tokokeza nje, akaelekezwa na mzee kwnye mtego, akalenga upande wa mtoto, badala ya kumuuwa, akamkwepa. Alpoulizwa vipi wewe? kasema, mnyama mwenyewe alikuwa anacheka, mi nikadhani yawezekana kuna maelewano wamekubaliana na baba.

Dawa ya kuacha Pombe

Mlevi nae akaenda kupata dawa ya kuacha pombe, akambiwa awe anameza vidonge viwili mara tatu kwa siku, akamuuliza dr, hizi dawa kwani zinamadhara nikimeza alafu nikanywa pombe?

dawa ya kuacha bangi

Mshikaji alienda kwa Dr kupata dawa ya kuacha bangi, dr akamwambia awe anameza mara tatu kwa siku, mshikaji akamuuliza niwe nameza baada ya kuvuta bangi au kabla?

kama Mvua inanyesha

Jamaa alikuwa Ktandani na mke wa mtu mwenyewe akarudi na kugonga Mlango Mke akamwambia Jamaa pitia dirishan Kimbia, jamaa akaanza kubisha eti nje Kuna Mvua, Mwanamke akamwambia Mme wangu ana hasira na ana Pisto, jamaa akachukua Nguo zake na kuruka dirishani na Kukimbia kufika Barabarani akakuta watu wengi wanakimbia wako kwenye Mashindano ya mbio nae akajiunga mmoja akamuulza mbona unakimbia Uchi? Jamaa akajibu napenda sana kukimbia hivi najisikia poa, mwingine akamwambia ndo ukimbie Nguo umebana kwapani? Akajbu sasa niziweke wapi? Mwingine akamuulza kwa hiyo kila ukiwa unakimbia unavaa Kondom? Jamaa huwa navaa kama Mvua inanyesha.

kufanyiwa usaili

Jost alikuwa anatafuta kazi sana... akaenda ofisi moja na kuanza kufanyiwa usaili,
Afisa: una akili timam
Jost: ndio, ninazo.
Afisa: 1 + 1 =?
Jost: 2
Afisa: nani alimuua Abraham Lincorin?
Jost: mhh! Sijui
Afisa: okey! Kalifanyie kazi hilo afu kesho urudi hapa...
Jost akaenda kwa rafik yake, akaulizwa umepata kazi?

Jost akajibu “ndio, tena nzito kweli, nashughulikia kesi ya mauaji.”