tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Sunday, February 14, 2016

Mwanamke

Wakati Tarime mwanamke anamnyang'anya Jambazi bunduki.....! Dar mwanamke anamkimbia mende!

Friday, February 12, 2016

Mke wangu

Jamaa kapiga simu kumuuliza sheikh.
Jamaa: Sheikh kila siku usiku nikishtuka kwenye usingizi naona nuru/mwanga inatoka kwenye uso wa mke wangu na yeye kajifunika blanket. Na nakuwa nakhofu kukamilisha usingizi wangu. Jee hii ni dalili ya kuwa mke wangu miongoni wa watu wema??

Sheikh: badilisha pin code yako ya simu maana mke wako anapekuwa simu yako wakati umelala

Thursday, February 11, 2016

Usikate miti

Je wajua???
Binadamu ndio kiumbe pekee awezaye kukata miti akatengeneza karatasi kisha juu ya karatasi akaandika "USIKATE MITI"

Sunday, February 7, 2016

Ubuyu

MUME: Vipi wife, leo utaratibu wa kuchagua nini kipikwe si unaendelea?

MKE: Kama kawaida mume wangu, ila leo majanga.

MUME: Kuna nini tena?

MKE: Juzi we si ulichagua pilau tukapika? Na jana mimi nikachagua mtori ukapikwa?

MUME: Ndiyo mke wangu.

MKE: Sasa leo zamu ya mwanao Junior., na ameshachagua hatuna budi kutii..

MUME: Kachagua nini?

MKE: Ubuyu!!