tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Sunday, April 17, 2016

Mmeo

Kuna Jamaa Kwenye Daladala Hapa Alikuwa Anaongea Na Simu....... Halooo Leo Sitaweza Kuja Nimepanda Gari Moja Na Mmeo...... Unaambiwa Wanaume Wote wenye Wake.... Wamemng'ang'ania Aoneshe Hiyo Namba Aliyokuwa Anaongea Nayo...... Sijui Kamalizana Nao Vipi Maana Mimi Nilishuka Kituo Kilichofuata.

Friday, April 8, 2016

Faraja

Ukikaa ukitafakari kuna milio mingi saana duniani ya gitaa,kinanda,pikipiki,gari etc.....lakini ule mlio m1 wakati ATM inatoa fedha ule grrrrr grrrr hua una faraja saana moyoni.... Daah pesa huyu

Wednesday, April 6, 2016

Unywaji pombe

Chukua tahadhari,

Unywaji pombe kupita kiasi hupelekea upungufu wa kumbukumbu na matatizo mengine mengine......... ambayo siyakumbuki vizuri!

Bahati iliyoje

BAHATI ILIOJE HII JAMANI.
××××××××××××××××××

Kuna siku nilikuwa maeneo ya Mjini kati
(City Center), nikaipenda suruali moja ya
shilingi 15,000/= na pesa sikuwa nayo
ikabidi niende kutoa kwenye ATM ya
Postal.
Nimefika pale sikukuta mtu hivyo
niliingia moja kwa moja, nimefika mle
ndani nikakuta Pesa Kibao zimemwagika
pale kwenye kitundu cha kutolea pesa,
ATM Card ilikuwepo pale imetokezea na
Pembeni kulikuwa na Pochi ya Kike
iliyoonekana kutuna vilivyo.
Kwa woga mimi huku nikitetemeka
mapigo ya moyo yakiwa yameongezeka
nikatizama nyuma yangu sikuona mtu,
nikachukua zile Pesa harakaharaka, ATM
na ile pochi.
Ile natoka nje kuna dada mmoja alikuwa
anakuja kwa kasi maeneo yale nikapata
uoga nikamuuliza "Samahani dada, kuna
kitu umesahau humu", yule dada
hakunijibu kitu kaingia kwenye chumba
cha ATM akachomeka Kadi kutoa hela
mi nikaondoka zangu fasta kuelekea
home.
Nimefika home nikajifungia ndani na
kuzibwaga zile pesa kitandani,
nikafungua wallet nikakuta imejaa
dollar, Vipodozi, iphone na ki-Nokia
kidogo cha tochi, ATM Card mbili za
Benki tofauti ambazo zilikuwa
zimezungushiwa karatasi iliyokuwa na
namba za siri za ATM zote, moyo
ukanilipuka paaaa!!! Nikaona bora
Nipumzike kwanza kitandani!!
Muda si mrefu ile iphone ikaanza kuita,
nilipoangalia halikutokea jina nikaona
bora nipokee nimsikilize anasemaje,
ilikuwa sauti ya kike iliyoongea kwa
huzuni kwa kubembeleza huku akilia na
alijitambulisha vizuri kuwa ile mali ni ya
kwake! Huruma ilinijia nikamwelekeza
nilipo aje kuchukua...
Hakuchukua muda akawa amefika nami
nikamkabidhi vitu vyote naye
akavihakiki na kukuta viko sana: Milioni
3 za Kibongo na Dollar 500. Dada
kanishukuru na kunipa ile Millioni 3 ya
kibongo mi nikazikataa kwasababu ni
mali yake na alizisahau tu.
Alinitoa hofu kwa kunisihi nichukue tu,
mi kama binadamu mwenyezi Mungu
atanilipa, nikakataa... Mwishowe
akaomba namba yangu na kuondoka
zake, akawa ameniacha ndani huku njaa
sasa nikaanza kuisikia, nilikuwa na buku
mbili nikaenda kula viepe kavu na soda
nikawa powa.
Sasa jana kanipigia simu kuwa anakuja
nimsubiri, dakika tano tu akanipigia tena
kuwa ameshafika yupo nje yupo ndani
ya Prado mpyaa nikaingia tukaondoka
akaenda kunionyesha kwake kisha
tukaelekea kwenye nyumba nyingine
iliyokuwa ndo imekamilika kujengwa
akaniambia hii itakuwa yako
akanikabidhi baadhi ya nyaraka na
funguo zote sikuamini...!!
Akanisindikiza kwangu, kufika home
ananiambia hiyo gari (Prado) nayo
ananiachia ni kwa mema tu
niliyomfanyia, ndani ya ile gari kulikuwa
na brifcase iliyokuwa na pesa
akaniambia pia hii pesa itakuwa yako ya
kuanzia maisha, na kumbe yule dada
alikuwa kanipenda akanikumbatia kwa
nguvu nikiwa pale kwenye seat oooh!!
umasikini baibai...
Akiwa kanikumbatia akihema kwa kasi
juu ya kifua changu. Mara nikahisi kubanwa na haja ndogo, nikakimbia fasta chooni na kuanza kukojoa, nasikia raaaha mkojo hauishi mara nikahisi mtu
akinishika begani na  kuniita kwa sauti.
"Anko ankoo we ankoo... amka unakojoa kitandaniii!!!".
"ALIKUWA MTOTO WA SISTA ALIKUWA
ANANIAMSHA !!"
Kumbe ndotooo mweeeh

Monday, April 4, 2016

Hali ya hewa

BOY: hellow baby

GIRL: Yes hubby

BOY: Unaona hali ya hewa kimvua kinashawishi...

GIRL: haswaaa tena kwa kilimo cha maharage....