tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Tuesday, October 25, 2011

unanionaje?

kulikuwa na wanandoa ambao ndio kwanza walikuwa wametoka kufunga ndoa karibuni. Siku moja mume alipotoka katika shughuli zake, mkewe akamwambia kuwa bomba la maji bafuni linavuna, mume akamjibu, mimi ni fundi bomba?
Siku nyingine mkewe akamwambia jamaa kuwa gari lake haliwaki hivyo akamtengenezee, jamaa kama kawaida yake na majibu yake, kwani mimi fundi magari?
Baada ya siku kadhaa kupita, mkewe kama kawaida akaleta shida nyingine kuwa paa linavuja. Kama kawaida akamjibu, unanionaje nimekaa kama fundi nyumba?
Siku iliyofuata alipotoka kazini alikuta kila kitu kimetengwenezwa na kuuliza kulikoni? Mkewe akajibu; nilipata mtu wa kunisaidia. Jamaa akajibu sawa nadaiwa shilingi ngapi? Mke akajibu. Hudaiwi hata shilingi kwa sababu alisema nimtengene keki au nifanye nae mapenzi kama malipo. Jamaa kwa wasiwasi akauliza. Umemtengenezea kekli ya aina gani? Mke akajibu, unanionaje, nimekaa kama mpika keki?