tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Sunday, September 4, 2011

ulevi ni noma.

mlevi alikuwa anahojiwa na police kwa kosa la kugonga na kuuwa watu nane.
Police: ilikuwaje ukagonga?
Mlevi: gari ilipata pacha tairi zote za mbele na gari ilikuwa kwenye mwendo mkali likanishinda na mbele yangu kulikuwa na kundi la watu kumi na upande mwingine wa barabara kulikuwa na mtu mmoja.
Police: kwanini ulifuata hilo kundi la watu badala ya kumfuata huyo mmoja?
Mlevi: nilimfuata huyo mmoja tatizo na yeye akakimbilia kwenye lile kundi la watu.

nani muongo?

wanandoa walikuwa wanaishi nyumba moja kwa muda mrefu, siku moja mke hakurudi nyumbani hadi asubuhi aliporudi. Mumewe alipomuuliza akajibu alilala kwa rafiki yake. Mumewe akawapigia simu marafiki zake kumi, wote wakajibu hakulala kwao.
Baada ya miezi michache mume nae akarudi asubuhi, mkewe nae alipo muuliza akajibu alilala kwa rafiki yake. Mkewe akaamua kuwapigia marafiki zake kumi, nane wakajibu alilala kwao wakati wawili wakasema amelala kwao na mpaka sasa bado yupo kwao.