tangazo one

tangazo one

Abidal

Abidal

karibuni

ni mara chache sana tunapata muda wa kujiuliza juu ya umuhimu wa watu waliotuzunguka, na maisha yetu yangekuwaje bila wao? wape nafasi na usisite kuwaambia jinsi unavyojisikia juu yao na umuhimu wao kwako. ASANTE KWA KUWA SEHEMU YA MAISHA YANGU.

Sunday, February 6, 2011

Nani Mwoga?

siku moja mtu na mkewe walikuwa wanabishana ni nani muoga kuliko mwenzie, mume akasema mke ndio muoga zaidi na mke akasema mume ndio muoga zaidi. wakaamua kuwauliza watoto wao.
Baba: jamani kati yangu mimi na mama yenu nani muoga zaidi?
Mtoto wa kwanza: mama ndio muoga kwa sababu anaogopa hata kutoka nje usiku baba akiwa amesafiri.
Mtoto wa pili: mimi naona baba ndio muoga zaidi, maana anaogopa hata kulala peke yake mama akiwa amesafiri anamuita dada (msichana wa kazi) analala nae hadi asubuhi.

Fundi Bomba.

fundi bomba alikuwa akitengeneza bomba la bafuni nyumbani kwa Zena. Zena akamfuata na kumwambia "naweza kuoga wakati wewe ukila chakula cha mcahana?"
Fundi akajibu: "bila shaka unaweza, ila tahadhari maji yasiingie kwenye chakula changu.

lina habari motomoto

Jonh alinunua gazeti na kwenda nalo nyumbani Asha, alipo fika akaliweka kwenye friji. Asha akashangazwa na jambo hilo na kuamua kumuuliza Jonh, "mbona umeweka gazeti kwenye  friji?"
Jonh: "wameandika lina habari motomoto, acha  zipoe kidigo nizisome.

Yesu Wangu

Mapadre wa kanisa moja walikuwa wanasafiri kwa basi lakini kabla ya kuanza safari yao kiongozi wao akawaambia , "mkiona mwanamke amevaa vibaya, anatembea kwa mwendo wa majaribu wa kishetani, msimwangalie sana bali mtake msaada wa Bwana kwa kusema 'Yesu Wangu'".
Safari ikaanza, baada ya dakika kadhaa padre mmoja akasema "Yesu Wangu". wenzake wote wakajeuka wakitizama nje na kumuuliza, "yupo wapi?"