umerud geto mida ya saa mbil ucku unaingia ndan ghafla unamuona nyoka kanyanyua shngo juu ana chzesha mkia na ki ulimi kinatoka toka nje.....Kwa ujasili unaamua kuchukua fmbo ili kumuua ...lkn ulivo jasiri zaid unaamua kufnga na mlango af funguo unatupia ktndan unajarbu kumdhuru lkn ghafla umeme unakatika
Hapo ndo utajua nobody can stop Reggae
tangazo one
Abidal
karibuni
Thursday, September 29, 2016
Nyoka
Wednesday, September 28, 2016
Daladala
Nimepanda daladala inavuja mpaka nikamshauri dereva aache kubeba abiria alime mchicha, hatuwezi kulowa hivi kwa daladala.
Sipendi uzembe mimi
Friday, September 23, 2016
Mwizi
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu
akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid
na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae
maana hta hela ya kula Jana sikua
nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu?
sipendagi utani na kitu hela mm!
Nani aliuwa Goliath
WAZAZI PELEKENI WATOTO SUNDAY SCHOOL PLEASE!!
TEACHER: Nani aliuwa Goliath......
STUDENT 1: Sio mimi.
STUDENT 2: Sikuwa shule jana. .
STUDENT 3: Mimi sijui.
(The Teacher went and told the Headmaster ati watoto wa hio class hawajui nani aliuwa Goliath.) ... ( headteacher goes to the class.)
HEADTEACHER: Nani aliuwa Goliath.
CLASS: Sio sisi.
H.TEACHER: Mkikosa kuniambia hii darasa itawaka moto.
CLASS: Hatujui teacher.
The H.TEACHER turns and asks the teacher....
"Uko sure Goliath aliuliwa na mtu wa hii
darasa?"
The teacher fainted...
Wednesday, September 21, 2016
Mke wangu
ETI NAMTONGOZA DEMU NAMPA NAMBA ALAFU ANAMPA BOYFRIEND WAKE AKANIPIGIA WE NANI UNAMTONGOZA MKE WANGU NIKAMJIBU MI MUHUDUMU WA GEST MWAMBIE AMESAHAU CHENCHI
Nimekunja sura
Leo kuna mtu nimemtolea uvivu ! amenikuta nimetulia akaniuliza mbona nimekunja sura ...nikamwambia nataka kuiweka kwenye bag.
Sipendangi ujinga mimi
Nilikula kuku
Unamualika binti luch harafu anakuja na maringo, eti oooh.....! Bebe ata sitakula wakati natoka home nilikula kuku....!!
Wewe kwa ugetlemen wako unamnunulia Whisky ya Jack Daniels ya elfu hamsini!
Baada ya binti wa watu kunywa mafunda kadhaa anatapika makande na mahindi ya kuchoma wallah...!!
Sasa apo inabidi umulize romantically .....!!
Sory baby...! Uko sure ulikula kuku au chakula cha kuku
Monday, September 19, 2016
Simu
Siku moja mfanyakazi alienda ofisini uku masikio
yake yote mawili yakiwa yamefungwa bandeji.
Bosi wake akamuuliza imekuaje kuhusu masikio
yako?. Jamaa akajibu.
"jana wakati napiga pasi nguo zangu, simu iliita, kwa
bahati mbaya badala ya kuweka simu sikioni nikaweka pasi".
"Sawa" Bosi akasema, "iyo ni kuhusu sikio moja, na
ilo sikio lingine ilikuaje?" Jamaa akajibu
"simu iliita tena!"
Wazazi wako
Unakutana na mdada ndani ya miezi miwili anataka aje waona wazazi wako. Dada, mi mwenyewe nlikaa miezi 9 tumboni kabla sijawaona wazazi wangu mwenyewe, usiniletee mapenzi ya Mwendokasi.
Sipendagi ujinga mimi
Nyumba za kupanga
UTAMU WA NYUMBA ZA KUPANGA!
Jana neighbor yangu alikuja
akaniambia nipunguze sauti ya radio
anataka kulala.
Leo anapika chapat na mimi
nmemwambia apunguze harufu ya
chapati nataka kula ugali. sipendi ujinga ajue.
Sunday, September 18, 2016
Vipofu
Jion ya jana niliwakuta vipofu wawili wakipigana
Basi nikapaza sauti na kusema ninamsapoti huyo aliye na kisu
Ghafla wote wakaanza kukimbia mmoja kule mwingne huko.
Ila hakuna aliyekuwa na kisu
Huwa sipendagi ugomvi mimi
Malaika
MTOTO: mama kwa nn unamuita mdogo angu malaika
MAMA: kwa sababu yeye ni mdogo sana na yupo kama malaika,
kwa nini umeuliza mwanangu?
MTOTO: nimemrusha dirishani nashangaa hajapaa
mama kazimia!!!
Friday, September 16, 2016
Mkopo
Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.
Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!
Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsApp...!
Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang'oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri.
Kisha nikaituma ile message
Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yake... Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.
Akatuma message akiniuliza...
Hao wanawake unawajuwa, ...mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweli...!
Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaa...!
Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaa...! Akaniandikia message nyingine....
...Nakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupe... Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuri...!
Nami nikamjibu...
Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipo...!
Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdai...!
Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaa.... Kama sio mie!
Wednesday, September 14, 2016
Daladala
Watu wengine bhanaa!!
Jana nilipanda daladala basi ile kaka yenu nikawa nimejiachia kuchati, kuna jamaa akawa anasoma msg zangu bila aibu yani anafutilia ninavyochati...
Basi nikasema ngoja nimtie Adabu.. Nikaamua nimtext jamaa "Oya Alex ngoja nilipue hii daladala muda ushafika" Yule jamaa akajirusha dirishani......
Na kavunjika miguu na kiuno........
Sipendi mambo ya kijinga mimi
Tuesday, September 13, 2016
Mwanamke
...ingekuwa vp dunia ingeongozwa na mwanamke kungekuwa hakuna vita, ungesikia tu.. Marekani aiongei na urusi, mara rwanda yainunia burundi, boko haramu yawapelekea umbea alshabaab, ethiopia yasusia misaada ya UN, mara djibout yamtuma balozi wake kuisuta sudan, waziri mkuu wa UK awachambe magaidi wa qt.. Yaani ingekuwa amani tu..!!
#shikamooni_wanawake